Rukia maudhui

circa 1050–1010 BC

Samuel & King Saul

Israel demands a king; Samuel anoints Saul, whose disobedience leads to his rejection as God chooses a man after his own heart.

810 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. 1 Samweli 1:26takriban 1165 KK

    naye Hana akamwambia Eli, “Hakika kama uishivyo, bwana wangu, mimi ndiye yule mama ambaye alisimama hapa karibu nawe akiomba kwa Bwana.

  2. 1 Samweli 1:27takriban 1165 KK

    Niliomba mtoto huyu, naye Bwana amenijalia kile nilichomwomba.

  3. 1 Samweli 1:28takriban 1165 KK

    Hivyo sasa ninamtoa kwa Bwana. Kwa maana maisha yake yote atakuwa ametolewa kwa Bwana.” Naye akamwabudu Bwana huko.

  4. 1 Samweli 2:1takriban 1165 KK

    Kisha Hana akaomba na kusema: “Moyo wangu wamshangilia Bwana, katika Bwana pembe yangu imeinuliwa juu. Kinywa changu chajisifu juu ya adui zangu, kwa kuwa naufurahia wokovu wako.

  5. 1 Samweli 2:2takriban 1165 KK

    “Hakuna yeyote aliye mtakatifu kama Bwana, hakuna mwingine zaidi yako; hakuna Mwamba kama Mungu wetu.

  6. 1 Samweli 2:3takriban 1165 KK

    “Msiendelee kusema kwa kiburi hivyo wala msiache vinywa vyenu kunena kwa kiburi, kwa kuwa Bwana ndiye Mungu ajuaye, na kwa yeye matendo hupimwa.

  7. 1 Samweli 2:4takriban 1165 KK

    “Pinde za mashujaa zimevunjika, lakini wale wanaojikwaa wamevikwa nguvu.

  8. 1 Samweli 2:5takriban 1165 KK

    Wale waliokuwa na chakula tele wamejikodisha wenyewe ili kupata chakula, lakini wale waliokuwa na njaa hawana njaa tena. Mwanamke yule aliyekuwa tasa amezaa watoto saba, lakini yule ambaye alikuwa na wana wengi amedhoofika.

  9. 1 Samweli 2:6takriban 1165 KK

    “Bwana huua na huleta uhai, hushusha chini mpaka kaburini na hufufua.

  10. 1 Samweli 2:7takriban 1165 KK

    Bwana humfanya mtu maskini naye hutajirisha, hushusha na hukweza.

  11. 1 Samweli 2:8takriban 1165 KK

    Humwinua maskini kutoka mavumbini na humwinua mhitaji kutoka lundo la majivu; huwaketisha pamoja na wakuu na kuwafanya warithi kiti cha enzi cha heshima. “Kwa kuwa misingi ya dunia ni ya Bwana; juu yake ameuweka ulimwengu.

  12. 1 Samweli 2:9takriban 1165 KK

    Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake, lakini waovu watanyamazishwa kwenye giza. “Si kwa nguvu mtu hushinda;

  13. 1 Samweli 2:10takriban 1165 KK

    wale wampingao Bwana wataharibiwa kabisa. Atapiga radi dhidi yao kutoka mbinguni; Bwana ataihukumu miisho ya dunia. “Atampa nguvu mfalme wake, na kuitukuza pembe ya mpakwa mafuta wake.”

  14. 1 Samweli 2:11takriban 1165 KK

    Kisha Elikana akaenda nyumbani Rama, lakini mtoto akahudumu mbele za Bwana chini ya kuhani Eli.

  15. 1 Samweli 2:12takriban 1165 KK

    Wana wa Eli walikuwa watu wabaya kabisa, hawakumheshimu Bwana.

  16. 1 Samweli 2:13takriban 1165 KK

    Basi ilikuwa desturi ya makuhani pamoja na watu kwamba kila mara yeyote anapotoa dhabihu na huku nyama ikiwa inachemshwa, mtumishi wa kuhani angalikuja na uma wenye meno matatu mkononi mwake.

  17. 1 Samweli 2:14takriban 1165 KK

    Angeutumbukiza huo uma kwenye sufuria au birika au sufuria kubwa au chungu, naye kuhani angalijichukulia mwenyewe chochote ambacho uma ungekileta. Hivi ndivyo walivyowatendea Waisraeli wote waliokuja Shilo.

  18. 1 Samweli 2:15takriban 1165 KK

    Lakini hata kabla mafuta ya mnyama hayajachomwa, mtumishi wa kuhani angalikuja na kusema kwa mtu ambaye alikuwa akitoa dhabihu, “Mpe kuhani nyama akaoke, kwani hatapokea nyama iliyochemshwa kutoka kwako, ila iliyo mbichi tu.”

  19. 1 Samweli 2:16takriban 1165 KK

    Kama mtu akimwambia, “Mafuta ya mnyama na yachomwe kwanza, ndipo uchukue chochote unachotaka,” mtumishi angalijibu, “Hapana, nipe sasa, kama huwezi nitaichukua kwa nguvu.”

  20. 1 Samweli 2:17takriban 1165 KK

    Hii Dhambi ya hawa vijana ilikuwa kubwa sana machoni pa Bwana, kwa kuwa waliitendea dhabihu ya Bwana kwa dharau.

  21. 1 Samweli 2:18takriban 1165 KK

    Lakini Samweli alikuwa akihudumu mbele za Bwana, kijana akivaa kisibau cha kitani.

  22. 1 Samweli 2:19takriban 1165 KK

    Kila mwaka mama yake alimshonea joho dogo na kumchukulia wakati alipokwea pamoja na mumewe kutoa dhabihu ya mwaka.

  23. 1 Samweli 2:20takriban 1165 KK

    Eli alikuwa akiwabariki Elikana na mkewe, akisema, “Bwana na akupe watoto kwa mwanamke huyu ili kuchukua nafasi ya yule aliyekuwa amemwomba na akamtoa kwa Bwana.” Kisha wakawa wanakwenda nyumbani.

  24. 1 Samweli 2:21takriban 1165 KK

    Bwana akawa mwenye neema kwa Hana, naye akapata mimba akazaa wana watatu na binti wawili. Wakati huo, kijana Samweli akaendelea kukua mbele za Bwana.

  25. 1 Samweli 2:22takriban 1165 KK

    Basi Eli, ambaye alikuwa mzee sana, alisikia kuhusu kila kitu ambacho wanawe walikuwa wakiwafanyia Israeli wote na jinsi walivyokutana kimwili na wanawake waliohudumu kwenye ingilio la Hema la Kukutania.