Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Kumcha Bwana ni utakatifu, nako kwadumu milele. Amri za Bwana ni za hakika, nazo zina haki.

  2. Kwa hizo mtumishi wako anaonywa, katika kuzishika kuna thawabu kubwa.

  3. Ni nani awezaye kutambua makosa yake? Nisamehe makosa yangu nisiyoyajua.

  4. Mlinde mtumishi wako na dhambi za makusudi, nazo zisinitawale. Ndipo nitakapokuwa sina lawama, wala sitakuwa na hatia ya kosa kubwa.

  5. Maneno ya kinywa changu na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu na Mkombozi wangu.

  6. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Bwana na akujibu unapokuwa katika dhiki, jina la Mungu wa Yakobo na liwe kinga yako.

  7. Tutashangilia kwa furaha utakaposhinda, tutainua bendera zetu kwa jina la Mungu wetu. Bwana na akupe haja zako zote.

  8. Sasa nafahamu kuwa Bwana humwokoa mpakwa mafuta wake, humjibu kutoka mbingu yake takatifu kwa nguvu za wokovu wa mkono wake wa kuume.

  9. Wengine wanatumaini magari ya vita, na wengine farasi, bali sisi tutalitumainia jina la Bwana, Mungu wetu.

  10. Ee Bwana, mwokoe mfalme! Tujibu tunapokuita!

  11. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, mfalme huzifurahia nguvu zako. Tazama jinsi ilivyo kuu furaha yake kwa ushindi unaompa!

  12. Ulimkaribisha kwa baraka tele na kumvika taji ya dhahabu safi kichwani pake.

  13. Alikuomba maisha, nawe ukampa, wingi wa siku milele na milele.

  14. Kutokana na ushindi uliompa, utukufu wake ni mkubwa, umeweka juu yake fahari na utukufu.

  15. Hakika umempa baraka za milele, umemfanya awe na furaha kwa shangwe ya uwepo wako.

  16. Kwa kuwa mfalme anamtumaini Bwana; kwa upendo usiokoma wa Aliye Juu Sana hatatikiswa.

  17. Mkono wako utawashika adui zako wote, mkono wako wa kuume utawakamata adui zako.

  18. Wakati utakapojitokeza utawafanya kama tanuru ya moto. Katika ghadhabu yake Bwana atawameza, moto wake utawateketeza.

  19. Utawaangamiza wazao wao kutoka duniani, uzao wao kutoka wanadamu.

  20. Ingawa watapanga mabaya dhidi yako na kutunga hila, hawawezi kufanikiwa,

  21. kwa kuwa utawafanya wakimbie utakapowalenga usoni pao kwa mshale kutoka kwenye upinde wako.

  22. Ee Bwana, utukuzwe katika nguvu zako, tutaimba na kusifu nguvu zako.

  23. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa utenzi wa “Kulungu wa Alfajiri.” Zaburi ya Daudi. Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Kwa nini uko mbali hivyo kuniokoa? Mbali hivyo na maneno ya kuugua kwangu?

  24. Ee Mungu wangu, ninalia mchana, lakini hunijibu, hata usiku, sinyamazi.

  25. Hata hivyo umesimikwa katika kiti cha enzi kama Uliye Mtakatifu; wewe ni sifa ya Israeli.