Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Kuhusu matendo ya wanadamu: kwa neno la midomo yako, nimejiepusha na njia za wenye jeuri.

  2. Hatua zangu zimeshikamana na njia zako; nyayo zangu hazikuteleza.

  3. Ee Mungu, ninakuita, kwa kuwa utanijibu, nitegee sikio lako na usikie ombi langu.

  4. Uonyeshe ajabu ya upendo wako mkuu, wewe uokoaye kwa mkono wako wa kuume wale wanaokukimbilia kutokana na adui zao.

  5. Nilinde kama mboni ya jicho lako, unifiche chini ya kivuli cha mbawa zako

  6. Inuka, Ee Bwana, pambana nao, uwaangushe, niokoe kutokana na waovu kwa upanga wako.

  7. Ee Bwana, mkono wako uniokoe na watu wa jinsi hii, kutokana na watu wa ulimwengu huu ambao fungu lao liko katika maisha haya. Na wapate adhabu ya kuwatosha. Watoto wao na wapate zaidi ya hayo, hukumu na iendelee kwa watoto wa watoto wao.

  8. Na mimi katika haki nitauona uso wako, niamkapo, nitaridhika kwa kuona sura yako.

  9. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi mtumishi wa Bwana aliyomwimbia Bwana wakati Bwana alipomwokoa mikononi mwa adui zake wote, na pia mkononi mwa Sauli. Alisema hivi: Nakupenda wewe, Ee Bwana, nguvu yangu.

  10. Bwana ni mwamba wangu, ngome yangu na mwokozi wangu, Mungu wangu ni mwamba, ambaye kwake ninakimbilia. Yeye ni ngao yangu na pembe ya wokovu wangu, ngome yangu.

  11. Ninamwita Bwana anayestahili kusifiwa, nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu.

  12. Katika shida yangu nalimwita Bwana, nilimlilia Mungu wangu anisaidie. Kutoka hekaluni mwake alisikia sauti yangu, kilio changu kikafika mbele zake, masikioni mwake.

  13. Dunia ilitetemeka na kutikisika, misingi ya milima ikatikisika, vilitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika.

  14. Moshi ukapanda kutoka puani mwake, moto uteketezao ukatoka kinywani mwake, makaa ya moto yawakayo yakatoka ndani mwake.

  15. Akazipasua mbingu akashuka chini, mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake.

  16. Alipanda juu ya kerubi akaruka, akapaa juu kwa mbawa za upepo.

  17. Alifanya giza kuwa kitu chake cha kujifunika, hema lake kumzunguka, mawingu meusi ya mvua ya angani.

  18. Kutokana na mwanga wa uwepo wake mawingu yalisogea, ikanyesha mvua ya mawe na umeme wa radi.

  19. Bwana alinguruma kutoka mbinguni, sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika.

  20. Aliipiga mishale yake na kutawanya adui, naam, umeme mwingi wa radi na kuwafukuza.

  21. Mabonde ya bahari yalifunuliwa, na misingi ya dunia ikawa wazi kwa kukaripia kwako, Ee Bwana, kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwako.

  22. Alinyoosha mkono kutoka juu na kunishika; alinitoa kutoka kilindi cha maji makuu.

  23. Walinikabili siku ya msiba wangu, lakini Bwana alikuwa msaada wangu.

  24. Alinileta nje mahali penye nafasi tele, akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami.

  25. Bwana alinitendea sawasawa na uadilifu wangu; sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa.