Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Self-Denial: Simon, Andrew, James, and John

5 mistari · 41 vipengele

Mistari kuhusu Simon, Andrew, James, and John

  1. Yesu alipokuwa akitembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona Simoni na Andrea nduguye wakizitupa nyavu zao baharini, kwa kuwa wao walikuwa wavuvi.

  2. Yesu akawaambia, “Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu.”

  3. Mara wakaacha nyavu zao, wakamfuata.

  4. Alipokwenda mbele kidogo, akamwona Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana nduguye, wakiwa kwenye mashua yao wakizitengeneza nyavu zao.

  5. Papo hapo akawaita, nao wakamwacha Zebedayo baba yao kwenye mashua pamoja na watumishi wa kuajiriwa, nao wakamfuata Yesu.