Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Sanitation

289 mistari · 10 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Katika viumbe hai vyote viishivyo kwenye maji, mnaweza kula yeyote aliye na mapezi na magamba.

  2. Lakini chochote kisicho na mapezi na magamba msile; kwenu ni najisi.

  3. Mnaweza kula ndege yeyote aliye safi.

  4. Lakini wafuatao msiwale: tai, furukombe, kipungu,

  5. kengewa mwekundu, kengewa mweusi, mwewe wa aina yoyote,

  6. kunguru wa aina yoyote,

  7. mbuni, kiruka-njia, dudumizi, kipanga wa aina yoyote,

  8. bundi, mumbi, bundi mkubwa,

  9. mwari, nderi, mnandi,

  10. korongo, koikoi wa aina yoyote, hudihudi na popo.

  11. Wadudu wote warukao kwa makundi ni najisi kwenu, msiwale.

  12. Lakini viumbe vyote vyenye mabawa vilivyo safi mwaweza kula.

  13. Msile kitu chochote mtakachokuta kimekufa. Mnaweza kumpa mgeni yeyote anayeishi katika mojawapo ya miji yenu, naye anaweza kula au mnaweza kumuuzia mtu wa nchi nyingine. Lakini ninyi ni watu watakatifu kwa Bwana Mungu wenu. Msitokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.

  14. Tumieni hiyo fedha kununua chochote ukitakacho: ngʼombe, kondoo, divai au kinywaji chochote chenye chachu au chochote mnachotaka. Kisha ninyi na wa nyumbani mwenu mtaila mbele za Bwana Mungu wenu na kufurahi.

  15. Itawapasa kumla ninyi wenyewe katika miji yenu. Wote wasio safi na walio safi kwa desturi za kiibada mwaweza kula kama vile mnavyokula paa au kulungu.

  16. Lakini kamwe msinywe damu; imwageni ardhini kama maji.

  17. Kama mtu ana hatia ya kosa linalompasa kuuawa naye akauawa, mwili wake utaangikwa mtini,

  18. kamwe msiuache mwili wake mtini usiku kucha. Hakikisheni mnauzika mwili wake siku ile ile, kwa sababu kila mtu anayeangikwa mtini yupo chini ya laana ya Mungu. Msiinajisi nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa kama urithi wenu.

  19. Ikiwa mtu amechafuka kwa sababu ya kutokwa na shahawa usiku, inampasa atoke nje ya kambi na kukaa huko.

  20. Lakini jioni ikikaribia ataoga, na baada ya jua kuzama ataingia tena kambini.

  21. Tengeni mahali nje ya kambi ambapo mnaweza kwenda kujisaidia.

  22. Kama sehemu ya vifaa vyenu kuweni na kitu cha kulimia, nanyi mnapojisaidia, chimba shimo na kisha funika kile kikutokacho.

  23. Pakitokea magonjwa ya ngozi ya kuambukiza, mwe waangalifu sana kufanya sawasawa na maagizo ya makuhani, ambao ni Walawi. Ni lazima mfuate kwa uangalifu yale niliyowaamuru.

  24. “Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mke wa baba yake, kwa maana anadharau malazi ya baba yake.”

  25. “Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mnyama yeyote.”