Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Remorse: General references

49 mistari · 1 kipengele

Mistari kuhusu General references

Chuja kwa kitabu
  1. Maisha yangu yamedhoofika kwa majonzi, naam, miaka yangu kwa kulia kwa maumivu makali; nguvu zangu zinaisha kwa ajili ya mateso, na mifupa yangu inachakaa.

  2. Kwa kuwa mishale yako imenichoma, na mkono wako umenishukia.

  3. Hakuna afya mwilini mwangu kwa sababu ya ghadhabu yako, mifupa yangu haina uzima kwa sababu ya dhambi zangu.

  4. Maovu yangu yamenifunika kama mzigo usiochukulika.

  5. Majeraha yangu yameoza na yananuka, kwa sababu ya upumbavu wa dhambi zangu.

  6. Nimeinamishwa chini na kushushwa sana, mchana kutwa nazunguka nikiomboleza.

  7. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Baada ya kukemewa na nabii Nathani kwa kuzini na Bathsheba. Ee Mungu, unihurumie, kwa kadiri ya upendo wako usiokoma, kwa kadiri ya huruma yako kuu, uyafute makosa yangu.

  8. Unioshe na uovu wangu wote na unitakase dhambi yangu.

  9. Kwa maana ninajua makosa yangu, na dhambi yangu iko mbele yangu daima.

  10. Dhidi yako, wewe peke yako, nimetenda dhambi na kufanya yaliyo mabaya machoni pako, ili uthibitike kuwa wa kweli unenapo, na kuwa na haki utoapo hukumu.

  11. Nioshe kwa hisopo, nami nitakuwa safi, unisafishe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.

  12. Unipe kusikia furaha na shangwe, mifupa uliyoiponda na ifurahi.

  13. Ufiche uso wako usizitazame dhambi zangu, na uufute uovu wangu wote.

  14. Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu.

  15. Usinitupe kutoka mbele zako wala kuniondolea Roho wako Mtakatifu.

  16. Unirudishie tena furaha ya wokovu wako, unipe roho ya utii, ili initegemeze.

  17. Ndipo nitakapowafundisha wakosaji njia zako, na wenye dhambi watakugeukia wewe.

  18. Ee Mungu, Mungu uniokoaye, niokoe na hatia ya kumwaga damu, nao ulimi wangu utaimba juu ya haki yako.

  19. Ee Bwana, fungua midomo yangu, na kinywa changu kitatangaza sifa zako.

  20. Wewe hupendezwi na dhabihu, au ningaliileta, hufurahii sadaka za kuteketezwa.

  21. Bali dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika, moyo uliovunjika wenye toba, Ee Mungu, hutaudharau.

  22. kwa kuwa mliyapuuza mashauri yangu yote na hamkukubali karipio langu,

  23. mimi nami nitawacheka katika maafa yenu, nitawadhihaki wakati janga litawapata:

  24. wakati janga litawapata kama tufani, wakati maafa yatawazoa kama upepo wa kisulisuli, wakati dhiki na taabu zitawalemea.

  25. Sasa basi wanangu, nisikilizeni; msiache ninalowaambia.