Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Pilgrims and Strangers: Long for their pilgrimage to end

9 mistari · 35 vipengele

Mistari kuhusu Long for their pilgrimage to end

  1. Nilisema, “Laiti ningekuwa na mbawa za njiwa! Ningeruka niende mbali kupumzika.

  2. Kwa maana twajua kama hema yetu ya dunia tunayoishi ikiharibiwa, tunalo jengo kutoka kwa Mungu, nyumba iliyo ya milele kule mbinguni, isiyojengwa kwa mikono ya wanadamu.

  3. Katika hema hii twalia kwa uchungu, tukitamani kuvikwa makao yetu ya mbinguni,

  4. kwa kuwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tena kuwa uchi.

  5. Kwa kuwa tukiwa bado katika hema hii twalia kwa uchungu na kulemewa, kwa sababu hatutaki kuvuliwa bali kuvikwa makao yetu ya mbinguni ili kwamba kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima.

  6. Basi Mungu ndiye alitufanya kwa ajili ya jambo lilo hilo naye ametupa Roho Mtakatifu kuwa amana, akituhakikishia ahadi ya kile kijacho.

  7. Kwa hiyo siku zote tunalo tumaini, hata ingawa tunajua kwamba wakati tukiwa katika mwili huu, tuko mbali na Bwana,

  8. kwa maana twaenenda kwa imani wala si kwa kuona.

  9. Naam, tunalo tumaini na ingekuwa bora zaidi kuuacha mwili huu na kwenda kukaa na Bwana.