Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Obedience to God: Christ, an example of

7 mistari · 45 vipengele

Mistari kuhusu Christ, an example of

  1. Lakini Yesu akamjibu, “Kubali hivi sasa, kwa maana ndivyo itupasavyo kwa njia hii kuitimiza haki yote.” Hivyo Yohana akakubali.

  2. Kumbukeni lile neno nililowaambia, ‘Hakuna mtumishi aliye mkuu kuliko bwana wake.’ Kama wamenitesa mimi, nanyi pia watawatesa. Kama wamelishika neno langu, watalishika na neno lenu pia.

  3. Kuweni na nia ile ile aliyokuwa nayo Kristo Yesu:

  4. Yeye, ingawa alikuwa na asili ya Mungu hasa, hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa kitu cha kushikilia,

  5. bali alijifanya si kitu, akachukua hali hasa na mtumwa, naye akazaliwa katika umbo la mwanadamu.

  6. Naye akiwa na umbo la mwanadamu, alijinyenyekeza, akatii hata mauti: naam, mauti ya msalaba!

  7. Ingawa alikuwa Mwana, alijifunza utiifu kutokana na mateso aliyoyapata,