Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Missionary Work By Ministers: Christ sent his disciples to labour in

13 mistari · 32 vipengele

Mistari kuhusu Christ sent his disciples to labour in

  1. Akawachagua kumi na wawili, ambao aliwaita mitume, ili wapate kuwa pamoja naye, na awatume kwenda kuhubiri

  2. Akawaita wale kumi na wawili, akawatuma wawili wawili, na kuwapa mamlaka kutoa pepo wachafu.

  3. Baada ya hayo, Bwana akawachagua wengine sabini na wawili, akawatuma wawili wawili katika kila mji na kila sehemu aliyokusudia kwenda baadaye.

  4. Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini watendakazi ni wachache. Kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno, ili apeleke watendakazi katika shamba lake la mavuno.

  5. Haya! nendeni. Ninawatuma kama wana-kondoo katikati ya mbwa mwitu.

  6. Msichukue mkoba, wala mfuko, wala viatu, na msimsalimu mtu yeyote njiani.

  7. “Mkiingia katika nyumba yoyote, kwanza semeni, ‘Amani iwe kwenu.’

  8. Kama kuna mtu wa amani humo, basi amani yenu itakuwa juu yake. La sivyo, itawarudia.

  9. Kaeni katika nyumba hiyo, mkila na kunywa kile watakachowapa, kwa sababu kila mtendakazi anastahili malipo yake. Msihamehame kutoka nyumba hadi nyumba.

  10. “Mkienda katika mji na watu wake wakawakaribisha, kuleni chochote kiwekwacho mbele yenu,

  11. waponyeni wagonjwa waliomo na waambieni: ‘Ufalme wa Mungu umekaribia.’

  12. Lakini mkiingia katika mji, nao hawakuwakaribisha, tokeni mwende katika barabara zake mkaseme:

  13. ‘Hata mavumbi ya mji wenu yaliyoshikamana na miguu yetu, tunayakungʼuta dhidi yenu. Lakini mjue kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia.’