Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Meekness

109 mistari · 29 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. “Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake.”

  2. Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakutishia, bali alijikabidhi kwa yeye ahukumuye kwa haki.

  3. Badala yake, kujipamba kwenu kuwe katika utu wenu wa moyoni, yaani uzuri usioharibika wa roho ya upole na utulivu, ambayo ni ya thamani sana machoni pa Mungu.

  4. Mtu huyo lazima aache uovu, akatende mema; lazima aitafute amani na kuifuatilia sana.

  5. Bali mtakaseni Kristo kuwa Bwana mioyoni mwenu. Siku zote mwe tayari kumjibu mtu yeyote atakayewauliza kuhusu sababu ya tumaini lililomo ndani yenu. Lakini fanyeni hivyo kwa upole na kwa heshima,

  6. Kwa sababu hii hasa, jitahidini sana katika imani yenu kuongeza wema; na katika wema, maarifa;

  7. katika maarifa, kiasi; katika kiasi, saburi; katika saburi, utauwa;

  8. katika utauwa, upendano wa ndugu; na katika upendano wa ndugu, upendo.

  9. Lakini hata malaika mkuu Mikaeli alipokuwa anashindana na ibilisi juu ya mwili wa Mose, hakuthubutu kumlaumu, bali alimwambia, “Bwana na akukemee!”