Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Meekness: General references

92 mistari · 29 vipengele

Mistari kuhusu General references

Chuja kwa kitabu
  1. Maskini watakula na kushiba, wale wamtafutao Bwana watamsifu: mioyo yenu na iishi milele!

  2. Huwaongoza wanyenyekevu katika haki, naye huwafundisha njia yake.

  3. Aache uovu, atende mema, aitafute amani na kuifuatilia.

  4. Bali wanyenyekevu watairithi nchi na wafurahie amani tele.

  5. Kutoka mbinguni ulitamka hukumu, nayo nchi ikaogopa, ikawa kimya:

  6. wakati wewe, Ee Mungu, ulipoinuka kuhukumu, kuwaokoa wote walioonewa katika nchi.

  7. Bwana huwahifadhi wanyenyekevu lakini huwashusha waovu mpaka mavumbini.

  8. Kwa maana Bwana anapendezwa na watu wake, anawavika wanyenyekevu taji ya wokovu.

  9. Mtu mwenye subira ana ufahamu mwingi, bali anayekasirika haraka huonyesha upumbavu.

  10. Jawabu la upole hugeuza ghadhabu, bali neno liumizalo huchochea hasira.

  11. Mtu mwepesi wa hasira huchochea ugomvi, bali mtu mvumilivu hutuliza ugomvi.

  12. Ni afadhali mtu mstahimilivu kuliko shujaa, mtu anayeitawala hasira yake kuliko yule autekaye mji.

  13. Afadhali kula ukoko mkavu ukiwa na amani na utulivu kuliko kukaa kwenye nyumba ya karamu kukiwa na magomvi.

  14. Hekima ya mtu humpa uvumilivu, ni kwa utukufu wake kusamehe makosa.

  15. Ni kwa heshima ya mtu kujitenga ugomvi, bali kila mpumbavu ni mwepesi kugombana.

  16. Kwa njia ya uvumilivu mtawala aweza kushawishiwa, nao ulimi laini waweza kuvunja mfupa.

  17. Wenye mzaha huuchochea mji, bali watu wenye hekima hugeuzia mbali hasira.

  18. Mwisho wa jambo ni bora kuliko mwanzo wake, uvumilivu ni bora kuliko kiburi.

  19. Kama hasira ya mtawala ikiwaka dhidi yako, usiache mahali pako, utulivu huweza kuzuia makosa mengi.

  20. bali kwa uadilifu atahukumu wahitaji, kwa haki ataamua wanyenyekevu wa dunia. Ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, kwa pumzi ya midomo yake atawaua waovu.

  21. Mara nyingine tena wanyenyekevu watafurahi katika Bwana, wahitaji watafurahi katika yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.

  22. Na akae peke yake awe kimya, kwa maana Bwana ameiweka juu yake.

  23. Na azike uso wake mavumbini bado panawezekana kuwa na matumaini.

  24. Na atoe shavu lake kwa yule ampigaye, na ajazwe na aibu.

  25. Je, watu wawili hutembea pamoja wasipokubaliana kufanya hivyo?