Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Instruction

179 mistari · 2 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Wewe ni mwema, unalotenda ni jema, nifundishe maagizo yako.

  2. Ingawa wenye majivuno wamenisingizia uongo, nitafuata mausia yako kwa moyo wangu wote.

  3. Mioyo yao ni katili na migumu, bali mimi napendezwa na sheria yako.

  4. Ilikuwa vyema mimi kupata shida ili nipate kujifunza maagizo yako.

  5. Sheria inayotoka kinywani mwako ina thamani kubwa kwangu kuliko maelfu ya vipande vya fedha na dhahabu.

  6. Mikono yako ilinifanya na kuniumba, nipe ufahamu niweze kujifunza amri zako.

  7. Wakuchao wafurahie wanaponiona, kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika neno lako.

  8. Ee Bwana, ninajua kwamba sheria zako ni za haki, katika uaminifu wako umeniadhibu.

  9. Upendo wako usiokoma uwe faraja yangu, sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako.

  10. Huruma yako na inijie ili nipate kuishi, kwa kuwa naifurahia sheria yako.

  11. Wenye majivuno na waaibishwe kwa kunikosea mimi bila sababu, lakini mimi nitatafakari juu ya mausia yako.

  12. Wale wakuchao na wanigeukie mimi, hao ambao wanazielewa sheria zako.

  13. Moyo wangu usiwe na lawama katika kutii maagizo yako, ili nisiaibishwe.

  14. Nafsi yangu inazimia kwa kutamani wokovu wako, lakini nimeweka tumaini langu katika neno lako.

  15. Macho yangu yamefifia, nikingoja ahadi yako; ninasema, “Utanifajiri lini?”

  16. Ingawa nimekuwa kama kiriba kwenye moshi, bado sijasahau maagizo yako.

  17. Mtumishi wako itampasa angoje mpaka lini? Ni lini utawaadhibu washtaki wangu?

  18. Wenye majivuno wananichimbia mashimo, kinyume na sheria yako.

  19. Amri zako zote ni za kuaminika; unisaidie, kwa sababu watu wananishtaki bila sababu.

  20. Walikaribia kabisa kunifuta kutoka uso wa dunia, lakini sijaacha mausia yako.

  21. Yahifadhi maisha yangu sawasawa na upendo wako, nami nitatii sheria za kinywa chako.

  22. Ee Bwana, neno lako ni la milele, linasimama imara mbinguni.

  23. Uaminifu wako unaendelea kwa vizazi vyote, umeiumba dunia, nayo inadumu.

  24. Sheria zako zinadumu hadi leo, kwa kuwa vitu vyote vinakutumikia.

  25. Kama nisingefurahia sheria yako, ningeangamia katika taabu zangu.