Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Instruction

179 mistari · 2 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Katika mwaka wa tatu wa utawala wa akatuma maafisa wake ambao ni: Ben-Haili, Obadia, Zekaria, Nethaneli na Mikaya ili kufundisha katika miji ya Yuda.

  2. Pamoja nao walikuwepo Walawi fulani nao ni: Shemaya, Nethania, Zebadia, Asaheli, Shemiramothi, Yehonathani, Adoniya, Tobia, Tob-Adonia, pamoja nao walikuwepo makuhani Elishama na Yehoramu.

  3. Wakafundisha Yuda yote, wakiwa wamechukua Kitabu cha Sheria ya Bwana wakazunguka miji yote ya Yuda na kufundisha watu.

  4. Nitafungua kinywa changu kwa mafumbo, nitazungumza mambo yaliyofichika, mambo ya kale:

  5. yale ambayo tuliyasikia na kuyajua, yale ambayo baba zetu walituambia.

  6. Hatutayaficha kwa watoto wao; tutakiambia kizazi kijacho matendo yastahiliyo sifa ya Bwana, uweza wake, na maajabu aliyoyafanya.

  7. Aliagiza amri kwa Yakobo na akaweka sheria katika Israeli, ambazo aliwaamuru baba zetu wawafundishe watoto wao,

  8. ili kizazi kijacho kizijue, pamoja na watoto ambao watazaliwa, nao pia wapate kuwaeleza watoto wao.

  9. Ndipo wangeweka tumaini lao kwa Mungu, nao wasingesahau matendo yake, bali wangalizishika amri zake.

  10. Ili wasifanane na baba zao, waliokuwa kizazi cha ukaidi na uasi, ambao roho zao hazikuwa na uaminifu kwake, ambao roho zao hazikumwamini.

  11. Wasiofanya lolote lililo baya, wanaoenenda katika njia zake.

  12. Umetoa maagizo yako ili tuyatii kwa ukamilifu.

  13. Laiti mwenendo wangu ungekuwa imara katika kuyatii maagizo yako!

  14. Hivyo mimi sitaaibishwa ninapozingatia amri zako zote.

  15. Nitakusifu kwa moyo mnyofu ninapojifunza sheria zako za haki.

  16. Nitayatii maagizo yako; usiniache kabisa.

  17. Kijana aifanye njia yake kuwa safi jinsi gani? Ni kwa kutii, akilifuata neno lako.

  18. Ninakutafuta kwa moyo wangu wote, usiniache niende mbali na amri zako.

  19. Nimelificha neno lako moyoni mwangu ili nisikutende dhambi.

  20. Sifa ni zako, Ee Bwana, nifundishe maagizo yako.

  21. Kwa midomo yangu nitasimulia sheria zote zinazotoka katika kinywa chako.

  22. Ninafurahia kufuata sheria zako kama mtu afurahiaye mali nyingi.

  23. Ninatafakari maagizo yako na kuziangalia njia zako.

  24. Ninafurahia maagizo yako, wala sitalipuuza neno lako.

  25. Mtendee mema mtumishi wako, nami nitaishi; nitalitii neno lako.