Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Harlot

47 mistari · 5 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. “Nina sadaka za amani nyumbani; leo nimetimiza nadhiri zangu.

  2. Kwa hiyo nimetoka nje kukulaki; nimekutafuta na nimekupata!

  3. Nimetandika kitanda changu kwa kitani za rangi kutoka Misri.

  4. Nimetia manukato kitanda changu kwa manemane, udi na mdalasini.

  5. Njoo, tuzame katika mapenzi mpaka asubuhi; tujifurahishe wenyewe kwa mapenzi!

  6. Mume wangu hayupo nyumbani; amekwenda safari ya mbali.

  7. Amechukua mkoba uliojazwa fedha na hatakuwepo nyumbani karibuni.”

  8. Kwa maneno laini yule mwanamke akampotosha; alimshawishi kwa maneno yake laini.

  9. Mara huyo kijana alimfuata yule mwanamke kama fahali aendaye machinjoni, kama kulungu aingiaye kwenye kitanzi,

  10. mpaka mshale umchome ini lake, kama ndege anayenaswa kwenye mtego, bila kujua itamgharimu maisha yake.

  11. Sasa basi wanangu, nisikilizeni; sikilizeni kwa makini nisemalo.

  12. Usiruhusu moyo wako ugeukie njia za huyo mwanamke, wala usitangetange katika mapito yake.

  13. Aliowaangusha ni wengi; aliowachinja ni kundi kubwa.

  14. Nyumba yake ni njia kuu iendayo kaburini, ielekeayo chini kwenye vyumba vya mauti.

  15. Mwanamke aitwaye Mpumbavu ana kelele; hana adabu na hana maarifa.

  16. Huketi kwenye mlango wa nyumba yake, juu ya kiti katika mahali pa juu sana pa mji,

  17. akiita wale wapitao karibu, waendao moja kwa moja kwenye njia yao.

  18. Anawaambia wale wasio na akili, “Wote ambao ni wajinga na waje hapa ndani!”

  19. “Maji yaliyoibiwa ni matamu; chakula kinacholiwa sirini ni kitamu!”

  20. Lakini hawajui hata kidogo kuwa wafu wako humo, kwamba wageni wake huyo mwanamke wako katika vilindi vya kuzimu.

  21. Wakati huo Tiro utasahauliwa kwa miaka sabini, muda wa maisha ya mfalme. Lakini mwisho wa miaka hiyo sabini, itakuwa kwa Tiro kama ilivyo katika wimbo wa kahaba:

  22. “Twaa kinubi, tembea mjini kote, ewe kahaba uliyesahauliwa; piga kinubi vizuri, imba nyimbo nyingi, ili upate kukumbukwa.”