Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Abraham: Children of

10 mistari · 39 vipengele

Mistari kuhusu Children of

  1. Hivyo Hagari akamzalia Abramu mwana, naye Abramu akamwita huyo mwana Hagari aliyemzalia, Ishmaeli.

  2. Sara akapata mimba, akamzalia Abrahamu mwana katika uzee wake, majira yale ya Mungu aliomwahidi.

  3. Abrahamu akamwita Isaki yule mwana ambaye Sara alimzalia.

  4. Abrahamu alioa mke mwingine, ambaye jina lake aliitwa Ketura.

  5. Huyu alimzalia Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua.

  6. Yokshani alikuwa baba wa Sheba na Dedani, wazao wa Dedani walikuwa Waashuri, Waletushi na Waleumi.

  7. Wana wa Midiani walikuwa Efa, Eferi, Hanoki, Abida na Eldaa. Hawa wote walikuwa uzao wa Ketura.

  8. Wana waliozaliwa na Ketura suria wa Abrahamu walikuwa: Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua. Wana wa Yokshani walikuwa: Sheba na Dedani.

  9. Wana wa Midiani walikuwa: Efa, Eferi, Hanoki, Abida na Eldaa. Wote hao walikuwa wa uzao wa Ketura.

  10. Abrahamu alikuwa baba wa Isaki. Wana wa Isaki walikuwa: Esau na Israeli.