Skip to content

Heth

12 mistari · 11 wanafamilia

Mistari inayomtaja Heth

  1. Kanaani alikuwa baba wa: Sidoni mzaliwa wake wa kwanza, Hethi,

  2. Ndipo Abrahamu akainuka kutoka pale penye maiti ya mke wake. Akazungumza na Wahiti, akasema,

  3. Wahiti wakamjibu Abrahamu,

  4. Abrahamu akainuka na akasujudu mbele ya wenyeji wa nchi, yaani Wahiti.

  5. Efroni Mhiti alikuwa ameketi miongoni mwa watu wake, akamjibu Abrahamu mbele ya Wahiti wote waliokuwepo katika lango la mji.

  6. Abrahamu akakubali masharti ya Efroni, akampimia ile fedha aliyotaja masikioni mwa Wahiti: Shekeli 400 za fedha kulingana na viwango vya uzito vilivyokuwa vikitumika wakati huo na wafanyabiashara.

  7. kwa Abrahamu kuwa mali yake mbele ya Wahiti wote waliokuwa wamekuja kwenye lango la mji.

  8. Hivyo Wahiti wakamkabidhi Abrahamu shamba pamoja na pango lililokuwa humo kuwa mahali pa kuzikia.

  9. Shamba ambalo Abrahamu alilinunua kwa Wahiti. Hapo ndipo Abrahamu alipozikwa pamoja na mkewe Sara.

  10. Kisha Rebeka akamwambia Isaki, “Nimechukia kuishi kwa sababu ya hawa wanawake wa Kihiti. Ikiwa Yakobo ataoa mke miongoni mwa wanawake wa nchi hii, wanawake wa Kihiti kama hawa, sitakuwa na faida kuendelea kuishi.”

  11. Shamba hilo na pango lililoko ndani yake lilinunuliwa kutoka kwa Wahiti.”

  12. Wana wa Kanaani walikuwa: Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi,