Rukia maudhui

circa 1446–1406 BC

The Wilderness Years

Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.

2,247 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Hesabu 7:80takriban 1490 KK

    sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

  2. Hesabu 7:81takriban 1490 KK

    fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

  3. Hesabu 7:82takriban 1490 KK

    mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

  4. Hesabu 7:83takriban 1490 KK

    maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Ahira mwana wa Enani.

  5. Hesabu 7:84takriban 1490 KK

    Hizi ndizo zilikuwa sadaka za viongozi wa Israeli madhabahu yalipowekwa wakfu, wakati yalitiwa mafuta: sahani kumi na mbili za fedha, bakuli kumi na mbili za fedha za kunyunyizia, na masinia kumi na mawili ya dhahabu.

  6. Hesabu 7:85takriban 1490 KK

    Kila sahani ya fedha ilikuwa na uzito wa shekeli 130, na kila bakuli la fedha la kunyunyizia lilikuwa na uzito wa shekeli sabini. Masinia yote kumi na mawili yalikuwa na uzito wa shekeli 2,400kulingana na shekeli ya mahali patakatifu.

  7. Hesabu 7:86takriban 1490 KK

    Sahani kumi na mbili za dhahabu zilizojazwa uvumba zilikuwa na uzito wa shekeli kumi kila moja, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. Kwa jumla, sahani za dhahabu zilikuwa na uzito wa shekeli 120.

  8. Hesabu 7:87takriban 1490 KK

    Jumla ya wanyama waliotolewa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa walikuwa fahali kumi na wawili wachanga, kondoo dume kumi na wawili na wana-kondoo dume kumi na wawili wa mwaka mmoja, pamoja na sadaka zao za nafaka. Mbuzi waume kumi na wawili walitolewa kwa ajili ya sadaka za dhambi.

  9. Hesabu 7:88takriban 1490 KK

    Jumla ya wanyama kwa ajili ya dhabihu ya sadaka ya amani walikuwa maksai ishirini na wanne, kondoo dume sitini, mbuzi dume wa mwaka mmoja sitini na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja sitini. Hizi ndizo zilikuwa sadaka zilizoletwa kwa ajili ya kuwekwa wakfu kwa madhabahu baada ya kutiwa mafuta.

  10. Hesabu 7:89takriban 1490 KK

    Mose alipoingia kwenye Hema la Kukutania kuzungumza na Bwana, alisikia sauti ikisema naye kutoka kati ya wale makerubi wawili waliokuwa juu ya kile kiti cha rehema, juu ya Sanduku la Ushuhuda. Mose akazungumza naye.

  11. Hesabu 8:1takriban 1490 KK

    Bwana akamwambia Mose,

  12. Hesabu 8:2takriban 1490 KK

    “Sema na Aroni umwambie, ‘Wakati utakapoziweka zile taa saba, zinatakiwa kuangaza eneo lililo mbele ya kinara cha taa.’ ”

  13. Hesabu 8:3takriban 1490 KK

    Aroni akafanya hivyo; akaziweka zile taa ili zielekee mbele kwenye kinara cha taa, kama vile Bwana alivyomwamuru Mose.

  14. Hesabu 8:4takriban 1490 KK

    Hivi ndivyo kinara cha taa kilivyotengenezwa: Kilitengenezwa kwa dhahabu iliyofuliwa, kuanzia kwenye kitako chake hadi kwenye maua yake. Kinara cha taa kilitengenezwa sawasawa kabisa na kielelezo ambacho Bwana alikuwa amemwonyesha Mose.

  15. Hesabu 8:5takriban 1490 KK

    Bwana akamwambia Mose:

  16. Hesabu 8:6takriban 1490 KK

    “Watwae Walawi kutoka miongoni mwa Waisraeli wengine na uwatakase kwa kawaida ya ibada.

  17. Hesabu 8:7takriban 1490 KK

    Ili kuwatakasa fanya hivi: Nyunyizia maji ya utakaso juu yao; kisha uwaambie wanyoe nywele kwenye mwili mzima, wafue nguo zao na hivyo wajitakase wenyewe.

  18. Hesabu 8:8takriban 1490 KK

    Waambie wamchukue fahali mchanga pamoja na sadaka yake ya nafaka ya unga laini uliochanganywa na mafuta; kisha utamchukua fahali mchanga wa pili kwa ajili ya sadaka ya dhambi.

  19. Hesabu 8:9takriban 1490 KK

    Walete Walawi mbele ya Hema la Kukutania na ukusanye jumuiya yote ya Waisraeli.

  20. Hesabu 8:10takriban 1490 KK

    Utawaleta Walawi mbele za Bwana, na Waisraeli wataweka mikono yao juu ya Walawi.

  21. Hesabu 8:11takriban 1490 KK

    Aroni atawaweka Walawi mbele za Bwana kama sadaka ya kuinua kutoka kwa Waisraeli, ili kwamba wawe tayari kuifanya kazi ya Bwana.

  22. Hesabu 8:12takriban 1490 KK

    “Baada ya Walawi kuweka mikono yao juu ya vichwa vya hao mafahali wawili, tumia mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi kwa Bwana, na mwingine kuwa sadaka ya kuteketezwa, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Walawi.

  23. Hesabu 8:13takriban 1490 KK

    Waambie hao Walawi wasimame mbele ya Aroni na wanawe, kisha wawatoe kama sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana.

  24. Hesabu 8:14takriban 1490 KK

    Kwa njia hii utakuwa umewatenga Walawi kutoka kwa Waisraeli wengine, nao Walawi watakuwa wangu.

  25. Hesabu 8:15takriban 1490 KK

    “Utakapokuwa umekwisha kuwatakasa Walawi na kuwatoa kama sadaka ya kuinuliwa, watakuja kufanya kazi yao katika Hema la Kukutania.