Rukia maudhui

circa AD 30–62

The Early Church

Pentecost ignites a movement; Peter, Paul, and countless others carry the gospel from Jerusalem to the ends of the earth.

1,007 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Matendo 13:12takriban 45 BK

    Yule mkuu wa kile kisiwa alipoona yaliyotukia, akaamini kwa sababu alistaajabishwa na mafundisho kuhusu Bwana.

  2. Matendo 13:13takriban 45 BK

    Kisha Paulo na wenzake wakasafiri toka Pafo wakafika Perga huko Pamfilia. Lakini, Yohana Marko akawaacha huko, akarejea Yerusalemu.

  3. Matendo 13:14takriban 45 BK

    Kutoka Perga wakaendelea hadi Antiokia ya Pisidia. Siku ya Sabato wakaingia ndani ya sinagogi, wakaketi.

  4. Matendo 13:15takriban 45 BK

    Baada ya Sheria ya Mose na Kitabu cha Manabii kusomwa, viongozi wa sinagogi wakawatumia ujumbe wakisema, “Ndugu, kama mna neno la kuwafariji watu hawa, tafadhali lisemeni.”

  5. Matendo 13:16takriban 45 BK

    Paulo akasimama, akawapungia mkono na kusema: “Enyi wanaume wa Israeli na ninyi nyote mnaomcha Mungu.

  6. Matendo 13:17takriban 45 BK

    Mungu wa watu hawa wa Israeli aliwachagua baba zetu, akawafanya kustawi walipokuwa huko Misri, kwa uwezo mwingi akawaongoza na kuwatoa katika nchi ile.

  7. Matendo 13:18takriban 45 BK

    Kwa muda wa miaka arobaini alivumilia matendo yao walipokuwa jangwani.

  8. Matendo 13:19takriban 45 BK

    Naye baada ya kuyaangamiza mataifa saba waliokuwa wakiishi katika nchi ya Kanaani, akawapa Waisraeli nchi yao iwe urithi wao.

  9. Matendo 13:20takriban 45 BK

    Haya yote yalichukua kama muda wa miaka 450. “Baada ya haya, Mungu akawapa waamuzi mpaka wakati wa nabii Samweli.

  10. Matendo 13:21takriban 45 BK

    Ndipo watu wakaomba wapewe mfalme, naye Mungu akawapa Sauli mwana wa Kishi wa kabila la Benyamini, aliyetawala kwa miaka arobaini.

  11. Matendo 13:22takriban 45 BK

    Baada ya kumwondoa Sauli katika ufalme, akawainulia Daudi kuwa mfalme wao. Mungu pia alimshuhudia, akisema, ‘Nimemwona Daudi mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayetimiza mapenzi yangu yote.’

  12. Matendo 13:23takriban 45 BK

    “Kutoka uzao wa mtu huyu, Mungu amewaletea Israeli Mwokozi Yesu, kama alivyoahidi.

  13. Matendo 13:24takriban 45 BK

    Kabla ya kuja kwa Yesu, Yohana alihubiri toba na ubatizo kwa watu wote wa Israeli.

  14. Matendo 13:25takriban 45 BK

    Yohana alipokuwa anakamilisha kazi yake, alisema: ‘Ninyi mnadhani mimi ni nani? Mimi si yeye. La hasha, lakini yeye yuaja baada yangu, ambaye mimi sistahili kufungua kamba za viatu vya miguu yake.’

  15. Matendo 13:26takriban 45 BK

    “Ndugu zangu, wana wa Abrahamu, nanyi watu wa Mataifa mnaomcha Mungu, ujumbe huu wa wokovu umeletwa kwetu.

  16. Matendo 13:27takriban 45 BK

    Kwa sababu wakaao Yerusalemu na viongozi wao hawakumtambua wala kuelewa maneno ya manabii yasomwayo kila Sabato, bali waliyatimiza maneno hayo kwa kumhukumu yeye.

  17. Matendo 13:28takriban 45 BK

    Ijapokuwa hawakupata sababu yoyote ya kumhukumu kifo, walimwomba Pilato aamuru auawe.

  18. Matendo 13:29takriban 45 BK

    Walipokwisha kufanya yale yote yaliyoandikwa kumhusu, walimshusha kutoka msalabani na kumzika kaburini.

  19. Matendo 13:30takriban 45 BK

    Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu.

  20. Matendo 13:31takriban 45 BK

    Naye kwa siku nyingi akawatokea wale waliokuwa pamoja naye kuanzia Galilaya hadi Yerusalemu. Nao sasa wamekuwa mashahidi wake kwa watu wetu.

  21. Matendo 13:32takriban 45 BK

    “Nasi tunawaletea habari njema, kwamba yale Mungu aliyowaahidi baba zetu

  22. Matendo 13:33takriban 45 BK

    sasa ameyatimiza kwetu sisi watoto wao, kwa kumfufua Yesu, kama ilivyoandikwa katika Zaburi ya pili: “ ‘Wewe ni Mwanangu; leo mimi nimekuzaa.’

  23. Matendo 13:34takriban 45 BK

    Kwa kuwa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu asioze kamwe, alitamka maneno haya: “ ‘Nitakupa wewe baraka takatifu zilizo za hakika nilizomwahidi Daudi.’

  24. Matendo 13:35takriban 45 BK

    Kama ilivyosemwa mahali pengine katika Zaburi, “ ‘Hutamwacha Aliye Mtakatifu wako kuona uharibifu.’

  25. Matendo 13:36takriban 45 BK

    “Kwa maana Daudi akiisha kulitumikia kusudi la Mungu katika kizazi chake, alilala; akazikwa pamoja na baba zake na mwili wake ukaoza.