Rukia maudhui

circa 930–586 BC

The Divided Kingdom

The kingdom splits into Israel and Judah; prophets warn of judgment as both nations slowly drift into idolatry and exile.

1,722 mistari · 3 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 2 Wafalme 21:8takriban 698 KK

    Sitaifanya tena miguu ya Waisraeli itangetange kutoka nchi niliyowapa baba zao, ikiwa watakuwa waangalifu kufanya kila kitu nilichowaamuru, na kuishika Sheria yote ambayo walipewa na Mose mtumishi wangu.”

  2. 2 Wafalme 21:9takriban 698 KK

    Lakini hawa watu hawakusikiliza. Manase akawapotosha, hivyo kwamba walifanya maovu mengi kuliko mataifa ambayo Bwana aliyaangamiza mbele ya Waisraeli.

  3. 2 Wafalme 21:10takriban 698 KK

    Bwana akasema kupitia watumishi wake manabii:

  4. 2 Wafalme 21:11takriban 698 KK

    “Manase mfalme wa Yuda ametenda dhambi hizi za kuchukiza. Amefanya maovu mengi kuliko Waamori waliokuwepo kabla yake, na ameiongoza Yuda katika dhambi kwa sanamu zake.

  5. 2 Wafalme 21:12takriban 698 KK

    Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli: Nitaleta maafa makubwa juu ya Yerusalemu na Yuda, kiasi kwamba masikio ya kila mmoja atakayesikia habari zake yatawasha.

  6. 2 Wafalme 21:13takriban 698 KK

    Nitanyoosha juu ya Yerusalemu kamba ya kupimia iliyotumika dhidi ya Samaria, na timazi iliyotumika dhidi ya nyumba ya Ahabu. Nitaifutilia mbali Yerusalemu kama mtu afutaye sahani, nikiifuta na kuifunikiza.

  7. 2 Wafalme 21:14takriban 698 KK

    Nitawakataa mabaki wa urithi wangu na kuwatia mikononi mwa adui zao. Watapokonywa mali zao na kutekwa nyara na adui zao wote,

  8. 2 Wafalme 21:15takriban 698 KK

    kwa sababu wametenda uovu machoni pangu na kunighadhibisha tangu siku baba zao walipotoka Misri mpaka siku ya leo.”

  9. 2 Wafalme 21:16takriban 698 KK

    Zaidi ya hayo, Manase pia alimwaga damu nyingi isiyo na hatia, hivi kwamba aliijaza Yerusalemu kutoka mwanzo hadi mwisho, mbali na dhambi ambayo alikuwa amesababisha Yuda kufanya, na hivyo wakatenda maovu machoni pa Bwana.

  10. 2 Wafalme 21:17takriban 698 KK

    Matukio mengine ya utawala wa Manase, na yote aliyoyafanya, pamoja na dhambi alizotenda, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda?

  11. 2 Wafalme 21:18takriban 643 KK

    Manase akalala pamoja na baba zake na akazikwa katika bustani ya jumba lake la kifalme, katika bustani ya Uza. Naye Amoni mwanawe akawa mfalme baada yake.

  12. 2 Wafalme 21:19takriban 643 KK

    Amoni alikuwa na miaka ishirini na miwili alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka miwili. Mamaye aliitwa Meshulemethi binti Haruzi, kutoka Yotba.

  13. 2 Wafalme 21:20takriban 643 KK

    Akatenda maovu machoni mwa Bwana, kama baba yake Manase alivyofanya.

  14. 2 Wafalme 21:21takriban 643 KK

    Akaenenda katika njia zote za baba yake, akaabudu sanamu ambazo baba yake aliziabudu na kuzisujudia.

  15. 2 Wafalme 21:22takriban 643 KK

    Akamwacha Bwana, Mungu wa baba zake, wala hakuenenda katika njia za Bwana.

  16. 2 Wafalme 21:23takriban 641 KK

    Watumishi wa Amoni wakafanya fitina juu yake, nao wakamuulia kwake nyumbani.

  17. 2 Wafalme 21:24takriban 641 KK

    Kisha watu wa nchi wakawaua wale wote waliokuwa wamefanya hila dhidi ya Mfalme Amoni. Wakamfanya Yosia mwanawe kuwa mfalme mahali pake.

  18. 2 Wafalme 21:25takriban 641 KK

    Matukio mengine ya utawala wa Amoni na yale aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda?

  19. 2 Wafalme 21:26takriban 641 KK

    Akazikwa kwenye kaburi lake katika bustani ya Uza. Naye Yosia mwanawe akawa mfalme baada yake.

  20. 2 Wafalme 22:1takriban 641 KK

    Yosia alikuwa na miaka minane alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka thelathini na mmoja. Mama yake aliitwa Yedida binti Adaya, kutoka Boskathi.

  21. 2 Wafalme 22:2takriban 641 KK

    Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana na kuenenda katika njia zote za Daudi baba yake. Hakugeuka upande wa kuume wala wa kushoto.

  22. 2 Wafalme 22:3takriban 642 KK

    Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wake, Mfalme Yosia akamtuma mwandishi Shafani mwana wa Azalia, mwana wa Meshulamu, kwenda katika Hekalu la Bwana. Akasema:

  23. 2 Wafalme 22:4takriban 642 KK

    “Panda uende kwa Hilkia, kuhani mkuu, umwambie ahesabu zile fedha ambazo zimeletwa katika Hekalu la Bwana, ambazo mabawabu wamekusanya kutoka kwa watu.

  24. 2 Wafalme 22:5takriban 642 KK

    Waambie waikabidhi kwa watu walioteuliwa kusimamia kazi ya Hekalu. Waamuru watu hawa wawalipe wafanyakazi ambao wanakarabati Hekalu la Bwana:

  25. 2 Wafalme 22:6takriban 642 KK

    wale maseremala, wajenzi na waashi. Waambie pia wanunue mbao na mawe yaliyochongwa ili kukarabati Hekalu.