Rukia maudhui

circa 1446 BC

Sinai & The Law

God meets Israel at Mount Sinai, reveals the Ten Commandments, and establishes the Tabernacle and the priestly covenant.

1,657 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Walawi 5:18takriban 1490 KK

    Atamletea kuhani kama sadaka ya hatia kondoo dume kutoka kundi lake, kondoo asiye na dosari na mwenye thamani halisi kifedha. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa kosa alilotenda bila kukusudia, naye atasamehewa.

  2. Walawi 5:19takriban 1490 KK

    Hii ni sadaka ya hatia; amekuwa na hatia kwa kufanya kosa dhidi ya Bwana.”

  3. Walawi 6:1takriban 1490 KK

    Bwana akamwambia Mose:

  4. Walawi 6:2takriban 1490 KK

    “Kama mtu yeyote akitenda dhambi, naye si mwaminifu kwa Bwana kwa kumdanganya jirani yake kuhusu kitu fulani alichokabidhiwa, au kimeachwa chini ya utunzaji wake, au kimeibwa, au kama akimdanganya,

  5. Walawi 6:3takriban 1490 KK

    au akiokota mali iliyopotea na akadanganya, au kuapa kwa uongo, au kama akitenda dhambi yoyote ambayo watu waweza kuitenda;

  6. Walawi 6:4takriban 1490 KK

    wakati akitenda dhambi hizo na kuwa mwenye hatia, ni lazima arudishe kile alichokuwa amekiiba au amekichukua kwa dhuluma, au alichokuwa amekabidhiwa, au mali iliyokuwa imepotea akaipata,

  7. Walawi 6:5takriban 1490 KK

    au chochote alichokuwa amekiapia kwa uongo. Lazima akirudishe kikamilifu, na aongeze sehemu ya tano ya thamani yake, vyote ampe mwenye mali siku ile anapeleka sadaka yake ya hatia.

  8. Walawi 6:6takriban 1490 KK

    Kisha kama adhabu lazima amletee kuhani, yaani kwa Bwana, kama sadaka yake ya hatia, kondoo dume asiye na dosari na mwenye thamani kamili kutoka kundi lake.

  9. Walawi 6:7takriban 1490 KK

    Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Bwana, naye atasamehewa kwa kosa lolote katika mambo hayo aliyoyatenda yaliyomfanya kuwa na hatia.”

  10. Walawi 6:8takriban 1490 KK

    Bwana akamwambia Mose:

  11. Walawi 6:9takriban 1490 KK

    “Mpe Aroni na wanawe agizo hili: ‘Haya ndiyo masharti kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa: Sadaka ya kuteketezwa itabaki kwenye moto juu ya madhabahu usiku kucha, mpaka asubuhi, nao moto lazima uwe unaendelea kuwaka juu ya madhabahu.

  12. Walawi 6:10takriban 1490 KK

    Kisha kuhani atavaa mavazi yake ya kitani, pamoja na nguo za ndani za kitani mwilini wake, na aondoe majivu ya sadaka ya kuteketezwa ambayo moto umeteketeza juu ya madhabahu, na kuyaweka kando ya madhabahu.

  13. Walawi 6:11takriban 1490 KK

    Kisha atayavua mavazi haya na kuvaa mengine, naye achukue yale majivu nje ya kambi na kuyapeleka mahali palipo safi kwa kawaida ya ibada.

  14. Walawi 6:12takriban 1490 KK

    Moto ulio juu ya madhabahu lazima uwe unaendelea kuwaka, kamwe usizimike. Kila asubuhi kuhani ataongeza kuni na kupanga sadaka ya kuteketezwa juu ya moto, na kuteketeza mafuta ya sadaka za amani juu yake.

  15. Walawi 6:13takriban 1490 KK

    Moto lazima uendelee kuwaka juu ya madhabahu mfululizo, kamwe usizimike.

  16. Walawi 6:14takriban 1490 KK

    “ ‘Haya ndiyo masharti ya sadaka ya nafaka: Wana wa Aroni wataileta mbele za Bwana, mbele za madhabahu.

  17. Walawi 6:15takriban 1490 KK

    Kuhani atachukua konzi ya unga laini na mafuta, pamoja na uvumba wote ulioko juu ya sadaka ya nafaka, ateketeze sehemu ya kumbukumbu juu ya madhabahu kama harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.

  18. Walawi 6:16takriban 1490 KK

    Aroni na wanawe watakula sehemu iliyobaki, lakini italiwa bila kutiwa chachu mahali patakatifu, nao wataila kwenye ua wa Hema la Kukutania.

  19. Walawi 6:17takriban 1490 KK

    Kamwe haitaokwa na chachu; nimewapa kama fungu lao la sadaka iliyotolewa kwangu kwa moto. Ni takatifu sana, kama vile ilivyo sadaka ya dhambi na ya hatia.

  20. Walawi 6:18takriban 1490 KK

    Kila mwanaume mzao wa Aroni aweza kuila. Ni fungu lake la kawaida la sadaka zilizotolewa kwa Bwana kwa moto kwa vizazi vijavyo. Chochote kinachozigusa kitakuwa kitakatifu.’ ”

  21. Walawi 6:19takriban 1490 KK

    Tena Bwana akamwambia Mose,

  22. Walawi 6:20takriban 1490 KK

    “Hii ni sadaka ambayo Aroni na wanawe wanapaswa kuleta kwa Bwana siku atakapotiwa mafuta: sehemu ya kumi ya efa ya unga laini kama sadaka ya kawaida ya nafaka. Nusu yake ataitoa asubuhi na nusu nyingine jioni.

  23. Walawi 6:21takriban 1490 KK

    Iandae kwa mafuta kwenye kikaango; ilete ikiwa imechanganywa vizuri, na utoe hiyo sadaka ya nafaka ikiwa imevunjwa vipande vipande kuwa harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.

  24. Walawi 6:22takriban 1490 KK

    Mwanawe atakayeingia mahali pake kama kuhani aliyetiwa mafuta ndiye atakayeiandaa. Ni fungu la kawaida la Bwana, nalo litateketezwa kabisa.

  25. Walawi 6:23takriban 1490 KK

    Kila sadaka ya nafaka ya kuhani itateketezwa kabisa; kamwe haitaliwa.”