Rukia maudhui

circa 1446 BC

Sinai & The Law

God meets Israel at Mount Sinai, reveals the Ten Commandments, and establishes the Tabernacle and the priestly covenant.

1,657 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Kutoka 31:3takriban 1491 KK

    nami nimemjaza Roho wa Mungu, pamoja na ustadi, uwezo na ujuzi katika aina zote za ufundi,

  2. Kutoka 31:4takriban 1491 KK

    ili kubuni michoro ya kupendeza katika ufundi wa dhahabu, fedha na shaba,

  3. Kutoka 31:5takriban 1491 KK

    kuchonga vito na kuvitia mahali, kufanya ufundi kwa mbao, na kujishughulisha na aina zote za ufundi.

  4. Kutoka 31:6takriban 1491 KK

    Tena nimemteua Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani, ili kumsaidia. Pia mafundi wote nimewapa ustadi wa kutengeneza kila kitu nilichokuamuru wewe:

  5. Kutoka 31:7takriban 1491 KK

    Hema la Kukutania, Sanduku la Ushuhuda pamoja na kiti cha rehema juu yake, pia na vifaa vyote vya kwenye hema,

  6. Kutoka 31:8takriban 1491 KK

    meza na vifaa vyake, kinara cha taa cha dhahabu safi na vifaa vyake vyote, madhabahu ya kufukizia uvumba,

  7. Kutoka 31:9takriban 1491 KK

    madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote, sinia na kinara chake,

  8. Kutoka 31:10takriban 1491 KK

    pamoja na mavazi matakatifu yaliyofumwa ya kuhani Aroni, na mavazi kwa ajili ya wanawe wakati wanahudumu katika kazi ya ukuhani,

  9. Kutoka 31:11takriban 1491 KK

    pia mafuta ya upako na uvumba wenye harufu nzuri kwa ajili ya Mahali Patakatifu. Watavitengeneza sawasawa kama vile nilivyokuagiza wewe.”

  10. Kutoka 31:12takriban 1491 KK

    Kisha Bwana akamwambia Mose,

  11. Kutoka 31:13takriban 1491 KK

    “Waambie Waisraeli, ‘Ninyi ni lazima mzishike Sabato zangu. Hii itakuwa ni ishara kati yangu na ninyi kwa ajili ya vizazi vijavyo, ili mpate kujua kwamba Mimi Ndimi Bwana, niwafanyaye ninyi watakatifu.

  12. Kutoka 31:14takriban 1491 KK

    “ ‘Mtaishika Sabato, kwa sababu ni takatifu kwenu. Yeyote atakayeinajisi lazima auawe, yeyote atakayefanya kazi siku hiyo lazima akafie mbali na watu wake.

  13. Kutoka 31:15takriban 1491 KK

    Kwa siku sita, mtafanya kazi, lakini siku ya saba ni Sabato ya kupumzika, takatifu kwa Bwana. Yeyote afanyaye kazi yoyote siku ya Sabato ni lazima auawe.

  14. Kutoka 31:16takriban 1491 KK

    Waisraeli wataishika Sabato, kuiadhimisha kwa vizazi vijavyo kuwa Agano la milele.

  15. Kutoka 31:17takriban 1491 KK

    Itakuwa ishara kati yangu na Waisraeli milele, kwa kuwa kwa muda wa siku sita Bwana aliumba mbingu na dunia, na siku ya saba akaacha kufanya kazi, akapumzika.’ ”

  16. Kutoka 31:18takriban 1491 KK

    Bwana alipomaliza kusema na Mose juu ya Mlima Sinai, Mungu akampa vile vibao viwili vya Ushuhuda, vibao vya mawe vilivyoandikwa kwa kidole cha Mungu.

  17. Kutoka 32:1takriban 1491 KK

    Watu walipoona kuwa Mose amekawia sana kushuka kutoka mlimani, walimkusanyikia Aroni na kumwambia, “Njoo, tutengenezee miungu itakayotutangulia. Kwa maana huyu jamaa yetu Mose aliyetupandisha kutoka Misri, hatujui jambo lililompata.”

  18. Kutoka 32:2takriban 1491 KK

    Aroni akawajibu, “Vueni vipuli vya dhahabu ambavyo wake zenu, wana wenu na binti zenu wamevaa, mkaniletee.”

  19. Kutoka 32:3takriban 1491 KK

    Kwa hiyo watu wote wakavua vipuli vyao, wakavileta kwa Aroni.

  20. Kutoka 32:4takriban 1491 KK

    Akavichukua vile vitu walivyomkabidhi, akavifanyiza kwa kusubu sanamu yenye umbo la ndama, akaichonga kwa kutumia chombo. Kisha wakasema, “Hii ndiyo miungu yenu, ee Israeli, iliyowapandisha kutoka Misri.”

  21. Kutoka 32:5takriban 1491 KK

    Aroni alipoona hili, akajenga madhabahu mbele ya yule ndama na kutangaza, “Kesho kutakuwa na sikukuu kwa Bwana.”

  22. Kutoka 32:6takriban 1491 KK

    Kwa hiyo siku iliyofuata watu wakaamka asubuhi na mapema na kutoa sadaka za kuteketeza na sadaka za amani. Baadaye watu wakaketi kula na kunywa, nao wakasimama, wakajizamisha katika sherehe.

  23. Kutoka 32:7takriban 1491 KK

    Kisha Bwana akamwambia Mose, “Shuka, kwa sababu watu wako, uliowatoa Misri, wamepotoka.

  24. Kutoka 32:8takriban 1491 KK

    Wamekuwa wepesi kugeuka na kuacha niliyowaamuru, na wamejitengenezea sanamu ya kuyeyusha yenye umbo la ndama. Wameisujudia na kuitolea dhabihu, nao wamesema, ‘Hii ndiyo miungu yenu, ee Israeli iliyokupandisha kutoka Misri.’ ”

  25. Kutoka 32:9takriban 1491 KK

    Bwana akamwambia Mose, “Nimeona watu hawa, nao ni watu wenye shingo ngumu.