Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Mioyo ya watu inamlilia Bwana. Ee ukuta wa Binti Sayuni, machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike.

  2. Inuka, lia usiku, zamu za usiku zianzapo; mimina moyo wako kama maji mbele za Bwana. Mwinulie yeye mikono yako kwa ajili ya maisha ya watoto wako, ambao wanazimia kwa njaa kwenye kila mwanzo wa barabara.

  3. “Tazama, Ee Bwana, ufikirie: Ni nani ambaye umepata kumtendea namna hii? Je, wanawake wakule wazao wao, watoto waliowalea? Je, kuhani na nabii auawe mahali patakatifu pa Bwana?

  4. “Vijana na wazee hujilaza pamoja katika mavumbi ya barabarani, wavulana wangu na wasichana wameanguka kwa upanga. Umewaua katika siku ya hasira yako, umewachinja bila huruma.

  5. “Kama ulivyoita siku ya karamu, ndivyo ulivyoagiza hofu kuu dhidi yangu kila upande. Katika siku ya hasira ya Bwana hakuna yeyote aliyekwepa au kupona; wale niliowatunza na kuwalea, adui yangu amewaangamiza.”

  6. Mimi ndiye mtu aliyeona mateso kwa fimbo ya ghadhabu yake.

  7. hakika, amegeuza mkono wake dhidi yangu tena na tena, mchana kutwa.

  8. Amefanya ngozi yangu na nyama yangu kuchakaa na ameivunja mifupa yangu.

  9. Amenizungushia ukuta ili nisiweze kutoroka, amenifunga kwa minyororo mizito.

  10. Hata ninapoita au kulia ili kuomba msaada, anakataa kupokea maombi yangu.

  11. Ameizuia njia yangu kwa mapande ya mawe, amepotosha njia zangu.

  12. ameniburuta kutoka njia, akanirarua na kuniacha bila msaada.

  13. Amevuta upinde wake na kunifanya mimi niwe lengo kwa ajili ya mishale yake.

  14. Alinichoma moyo wangu kwa mishale iliyotoka kwenye podo lake.

  15. Amenijaza kwa majani machungu na kunishibisha kwa nyongo.

  16. Amevunja meno yangu kwa changarawe, amenikanyagia mavumbini.

  17. Kwa hiyo nasema, “Fahari yangu imeondoka na yale yote niliyokuwa nimetarajia kutoka kwa Bwana.”

  18. Kwa sababu ya upendo mkuu wa Bwana, hatuangamii, kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe.

  19. Ni mpya kila asubuhi, uaminifu wako ni mkuu.

  20. Nimeiambia nafsi yangu, “Bwana ni fungu langu, kwa hiyo nitamngojea.”

  21. Bwana ni mwema kwa wale ambao tumaini lao ni kwake, kwa yule ambaye humtafuta;

  22. ni vyema kungojea kwa utulivu kwa ajili ya wokovu wa Bwana.

  23. Na atoe shavu lake kwa yule ampigaye, na ajazwe na aibu.

  24. Kwa kuwa watu hawakatiliwi mbali na Bwana milele.

  25. Ingawa huleta huzuni, ataonyesha huruma, kwa kuwa upendo wake usiokoma ni mkuu.