Rukia maudhui

God

11,427 mistari · 2 wanafamilia

Mistari inayomtaja God

Chuja kwa kitabu
  1. Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, nithibitishe katika haki, maana nimeishi maisha yasiyo na lawama; nimemtumainia Bwana bila kusitasita.

  2. Ee Bwana, unijaribu, unipime, uuchunguze moyo wangu na mawazo yangu;

  3. kwa maana upendo wako uko mbele yangu daima, nami natembea siku zote katika kweli yako.

  4. Ninanawa mikono yangu kwa kuwa sina hatia, naikaribia madhabahu yako, Ee Bwana,

  5. nikitangaza sifa yako kwa sauti kubwa, huku nikisimulia matendo yako ya ajabu.

  6. Ee Bwana, naipenda nyumba yako mahali unakoishi, mahali ambapo utukufu wako hukaa.

  7. Miguu yangu imesimama katika uwanja tambarare; katika kusanyiko kuu nitamsifu Bwana.

  8. Zaburi ya Daudi. Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, nimhofu nani?

  9. Jambo moja ninamwomba Bwana, hili ndilo ninalolitafuta: niweze kukaa nyumbani mwa Bwana siku zote za maisha yangu, niutazame uzuri wa Bwana na kumtafuta hekaluni mwake.

  10. Kwa kuwa siku ya shida, atanihifadhi salama katika maskani yake, atanificha uvulini mwa hema yake na kuniweka juu kwenye mwamba.

  11. Kisha kichwa changu kitainuliwa juu ya adui zangu wanaonizunguka. Katika maskani yake nitatoa dhabihu kwa kelele za shangwe; nitamwimbia Bwana na kumsifu.

  12. Isikie sauti yangu nikuitapo, Ee Bwana, unihurumie na unijibu.

  13. Moyo wangu unasema kuhusu wewe, “Utafute uso wake!” Uso wako, Bwana “Nitautafuta.”

  14. Usinifiche uso wako, usimkatae mtumishi wako kwa hasira; wewe umekuwa msaada wangu. Usinikatae wala usiniache, Ee Mungu Mwokozi wangu.

  15. Hata kama baba yangu na mama wakiniacha, Bwana atanipokea.

  16. Nifundishe njia yako, Ee Bwana, niongoze katika njia iliyonyooka kwa sababu ya watesi wangu.

  17. Nami bado nina tumaini hili: nitauona wema wa Bwana katika nchi ya walio hai.

  18. Mngojee Bwana, uwe hodari na mwenye moyo mkuu, nawe, umngojee Bwana.

  19. Zaburi ya Daudi. Ninakuita wewe, Ee Bwana, Mwamba wangu; usiwe kwangu kama kiziwi. Kwa sababu ukinyamaza nitafanana na walioshuka shimoni.

  20. Sikia kilio changu unihurumie ninapokuita kwa ajili ya msaada, niinuapo mikono yangu kuelekea Patakatifu pa Patakatifu pako.

  21. Kwa kuwa hawaheshimu kazi za Bwana, na yale ambayo mikono yake imetenda, atawabomoa na kamwe hatawajenga tena.

  22. Bwana asifiwe, kwa maana amesikia kilio changu nikimwomba anihurumie.

  23. Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu, moyo wangu umemtumaini yeye, nami nimesaidiwa. Moyo wangu unarukaruka kwa furaha nami nitamshukuru kwa wimbo.

  24. Bwana ni nguvu ya watu wake, ngome ya wokovu kwa mpakwa mafuta wake.

  25. Waokoe watu wako na uubariki urithi wako; uwe mchungaji wao na uwabebe milele.