God
Mistari inayomtaja God
Zaburi ya Daudi. Mpeni Bwana, enyi mashujaa, mpeni Bwana utukufu na nguvu.
Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake; mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake.
Sauti ya Bwana iko juu ya maji; Mungu wa utukufu hupiga radi, Bwana hupiga radi juu ya maji makuu.
Sauti ya Bwana ina nguvu; sauti ya Bwana ni tukufu.
Sauti ya Bwana huvunja mierezi; Bwana huvunja vipande vipande mierezi ya Lebanoni.
Sauti ya Bwana hupiga kwa miali ya umeme wa radi.
Sauti ya Bwana hutikisa jangwa; Bwana hutikisa Jangwa la Kadeshi.
Sauti ya Bwana huzalisha ayala, na huuacha msitu wazi. Hekaluni mwake wote wasema, “Utukufu!”
Bwana huketi akiwa ametawazwa juu ya gharika; Bwana ametawazwa kuwa Mfalme milele.
Bwana huwapa watu wake nguvu; Bwana huwabariki watu wake kwa kuwapa amani.
Utenzi wa kuweka wakfu hekalu. Zaburi ya Daudi. Nitakutukuza wewe, Ee Bwana, kwa kuwa umeniinua kutoka vilindi, na hukuacha adui zangu washangilie juu yangu.
Ee Bwana, Mungu wangu, nilikuita unisaidie na wewe umeniponya.
Ee Bwana, umenitoa Kuzimu, umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti.
Mwimbieni Bwana, enyi watakatifu wake; lisifuni jina lake takatifu.
Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi, bali upendo wake hudumu siku zote. Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha, lakini asubuhi kukawa na furaha.
Ee Bwana, uliponijalia, uliuimarisha mlima wangu, lakini ulipouficha uso wako nilifadhaika.
Kwako wewe, Ee Bwana, niliita, kwa Bwana niliomba rehema:
“Kuna faida gani katika kuangamia kwangu? Katika kushuka kwangu shimoni? Je, mavumbi yatakusifu? Je, yatatangaza uaminifu wako?
Ee Bwana, unisikie na kunihurumia, Ee Bwana, uwe msaada wangu.”
Uligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza, ulinivua nguo za gunia ukanivika shangwe,
ili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya. Ee Bwana Mungu wangu, nitakushukuru milele.
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, nimekukimbilia wewe, usiache nikaaibika kamwe, kwa haki yako uniokoe.
Nitegee sikio lako, uje uniokoe haraka; uwe kwangu mwamba wa kimbilio, ngome imara ya kuniokoa.
Kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu, uniongoze na kunilinda kwa ajili ya jina lako.
Uniepushe na mtego niliotegewa, maana wewe ndiwe kimbilio langu.