God
Mistari inayomtaja God
Mwimbieni wimbo mpya; pigeni kwa ustadi, na mpaze sauti za shangwe.
Maana neno la Bwana ni haki na kweli, ni mwaminifu kwa yote atendayo.
Bwana hupenda uadilifu na haki; dunia imejaa upendo wake usiokoma.
Kwa neno la Bwana mbingu ziliumbwa, jeshi lao la angani kwa pumzi ya kinywa chake.
Ameyakusanya maji ya bahari kama kwenye chungu; vilindi vya bahari ameviweka katika ghala.
Dunia yote na imwogope Bwana, watu wote wa dunia wamche.
Kwa maana Mungu alisema, na ikawa, aliamuru na ikasimama imara.
Bwana huzuia mipango ya mataifa, hupinga makusudi ya mataifa.
Lakini mipango ya Bwana inasimama imara milele, makusudi ya moyo wake kwa vizazi vyote.
Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, watu ambao aliwachagua kuwa urithi wake.
Kutoka mbinguni Bwana hutazama chini na kuwaona wanadamu wote;
kutoka maskani mwake huwaangalia wote wakaao duniani:
yeye ambaye huumba mioyo yao wote, ambaye huangalia kila kitu wanachokitenda.
Lakini macho ya Bwana yako kwa wale wamchao, kwa wale tumaini lao liko katika upendo wake usio na kikomo,
Sisi tunamngojea Bwana kwa matumaini, yeye ni msaada wetu na ngao yetu.
Mioyo yetu humshangilia, kwa maana tunalitumainia jina lake takatifu.
Upendo wako usio na mwisho ukae juu yetu, Ee Bwana, tunapoliweka tumaini letu kwako.
Zaburi ya Daudi, alipojifanya mwendawazimu mbele ya Abimeleki, ambaye alimfukuza, naye akaondoka. Nitamtukuza Bwana nyakati zote, sifa zake zitakuwa midomoni mwangu siku zote.
Nafsi yangu itajisifu katika Bwana, walioonewa watasikia na wafurahi.
Mtukuzeni Bwana pamoja nami, naam, na tulitukuze jina lake pamoja.
Nilimtafuta Bwana naye akanijibu, akaniokoa kwenye hofu zangu zote.
Wale wamtazamao hutiwa nuru, nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe.
Maskini huyu alimwita Bwana, naye akamsikia, akamwokoa katika taabu zake zote.
Malaika wa Bwana hufanya kituo akiwazunguka wale wamchao, naye huwaokoa.
Onjeni mwone kwamba Bwana ni mwema, heri mtu yule anayemkimbilia.