Skip to content
Hesabu 13:1-25

Hesabu 13:1-25

1
Bwana akamwambia Mose,
2
“Watume baadhi ya watu wakaipeleleze nchi ya Kanaani, ambayo ninawapa Waisraeli. Kutoka kwa kila kabila la baba zao, tuma mmoja wa viongozi wao.”
3
Hivyo kwa agizo la Bwana Mose akawatuma kutoka Jangwa la Parani. Wote walikuwa viongozi wa Waisraeli.
4
Haya ndiyo majina yao: kutoka kabila la Reubeni, Shamua mwana wa Zakuri;
5
kutoka kabila la Simeoni, Shafati mwana wa Hori;
6
kutoka kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune;
7
kutoka kabila la Isakari, Igali mwana wa Yosefu;
8
kutoka kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni;
9
kutoka kabila la Benyamini, Palti mwana wa Rafu;
10
kutoka kabila la Zabuloni, Gadieli mwana wa Sodi,
11
kutoka kabila la Manase (kabila la Yosefu), Gadi mwana wa Susi;
12
kutoka kabila la Dani, Amieli mwana wa Gemali;
13
kutoka kabila la Asheri, Sethuri mwana wa Mikaeli;
14
kutoka kabila la Naftali, Nabi mwana wa Wofsi;
15
kutoka kabila la Gadi, Geueli mwana wa Maki.
16
Haya ndiyo majina ya watu ambao Mose aliwatuma kuipeleleza nchi. (Mose akampa Hoshea mwana wa Nuni jina Yoshua.)
17
Mose alipowatuma wakaipeleleze Kanaani, alisema, “Pandeni kupitia Negebu, mwende mpaka nchi ya vilima.
18
Mwone nchi ni ya namna gani, na kama watu waishio humo wana nguvu au ni wadhaifu, iwapo ni wachache au wengi.
19
Wanaishi katika nchi ya namna gani? Je, ni nzuri au mbaya? Wanaishi katika miji ya namna gani? Je, haina kuta au ngome?
20
Ardhi iko aje? Ina rutuba au la? Je, kuna miti ndani yake au la? Jitahidini kadiri mwezavyo kuleta baadhi ya matunda ya nchi.” (Ulikuwa msimu wa kuiva zabibu za kwanza.)
21
Hivyo wakapanda na kuipeleleza nchi kutoka Jangwa la Sini hadi Rehobu, kuelekea Lebo-Hamathi.
22
Wakapanda kupitia Negebu hadi wakafika Hebroni, mahali ambapo Ahimani, Sheshai na Talmai, wazao wa Anaki, waliishi. (Hebroni ulikuwa umejengwa miaka saba kabla ya mji wa Soani ulioko Misri.)
23
Walipofika katika Bonde la Eshkoli, walivunja tawi lililokuwa na kishada kimoja cha zabibu. Wawili wao wakalichukua lile tawi kwenye mti, pamoja na komamanga na tini.
24
Eneo lile likaitwa Bonde la Eshkoli kwa sababu ya kile kishada cha zabibu ambacho Waisraeli walikikata huko.
25
Mwishoni mwa siku arobaini wakarudi kutoka kuipeleleza nchi.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options