Skip to content
Mathayo 26:1-16

Mathayo 26:1-16

1
Yesu alipomaliza kusema hayo yote, akawaambia wanafunzi wake,
2
“Kama mnavyojua, baada ya siku mbili itakuwa Pasaka, naye Mwana wa Adamu atasalitiwa ili asulubiwe.”
3
Basi viongozi wa makuhani na wazee wa watu wakakusanyika katika jumba la utawala la kuhani mkuu, jina lake Kayafa.
4
Wakafanya shauri ili kumkamata Yesu kwa siri na kumuua.
5
Lakini wakasema, “Isiwe wakati wa Sikukuu, kusitokee ghasia miongoni mwa watu.”
6
Yesu alikuwa Bethania nyumbani mwa Simoni aliyekuwa na ukoma,
7
naye mwanamke mmoja akamjia akiwa na chupa ya marhamu yenye manukato ya thamani kubwa; akayamimina kichwani mwa Yesu alipokuwa ameketi mezani kula chakula.
8
Lakini wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, “Upotevu huu wote ni wa nini?
9
Manukato haya yangeuzwa kwa bei kubwa, na fedha hizo wakapewa maskini.”
10
Yesu, akijua jambo hili, akawaambia, “Mbona mnamsumbua huyu mwanamke? Yeye amenitendea jambo zuri sana.
11
Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini mimi hamtakuwa nami siku zote.
12
Alipomiminia haya manukato kwenye mwili wangu, amefanya hivyo ili kuniandaa kwa ajili ya maziko yangu.
13
Amin, nawaambia, mahali popote ulimwenguni ambapo hii Injili itahubiriwa, jambo hili alilolitenda huyu mwanamke litatajwa pia kwa ukumbusho wake.”
14
Kisha mmojawapo wa wale kumi na wawili, aitwaye Yuda Iskariote, alikwenda kwa viongozi wa makuhani
15
na kuuliza, “Mtanipa nini nikimtia Yesu mikononi mwenu?” Wakamlipa vipande thelathini vya fedha.
16
Tangu wakati huo Yuda akawa anatafuta wakati uliofaa wa kumsaliti Yesu.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Reading Width 90 chars

Options