Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Zipporah: Separates from Moses, is brought again to him by her father

5 mistari · 4 vipengele

Mistari kuhusu Separates from Moses, is brought again to him by her father

  1. Baada ya Mose kumrudisha mkewe Sipora, Yethro baba mkwe wake alimpokea

  2. pamoja na wanawe wawili. Jina la mmoja aliitwa Gershomu, kwa kuwa Mose alisema, “Nimekuwa mgeni katika nchi ya kigeni.”

  3. Mwingine aliitwa Eliezeri, kwa kuwa alisema, “Mungu wa baba yangu alikuwa msaada wangu, akaniokoa kutoka upanga wa Farao.”

  4. Yethro, baba mkwe wa Mose, pamoja na wana wawili wa Mose na mkewe, wakamjia Mose huko jangwani, mahali alipokuwa amepiga kambi karibu na mlima wa Mungu.

  5. Yethro alikuwa ametuma ujumbe kwake Mose, kusema, “Mimi Yethro baba mkwe wako ninakuja kwako pamoja na mke wako na wanao wawili.”