Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Watchfulness: Danger of remissness in

8 mistari · 28 vipengele

Mistari kuhusu Danger of remissness in

  1. Lakini kama huyo mtumishi ni mwovu, naye akasema moyoni mwake, ‘Bwana wangu atakawia muda mrefu,’

  2. kisha akaanza kuwapiga watumishi wenzake, na kula na kunywa pamoja na walevi.

  3. Basi bwana wa mtumishi huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyoijua.

  4. Atamkata vipande vipande na kumweka katika sehemu moja pamoja na wanafiki, mahali ambako kutakuwa ni kulia na kusaga meno.

  5. Bwana arusi alipokawia kuja wale wanawali wote wakasinzia na kulala.

  6. Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara, ‘Tupatieni mafuta yenu kidogo; taa zetu zinazimika.’

  7. “Lakini yeye bwana arusi akawajibu, ‘Amin, amin nawaambia, siwajui ninyi!’

  8. Kumbuka basi yale uliyoyapokea na kuyasikia, yatii na ukatubu. Lakini usipoamka, nitakuja kama mwizi wala hutajua saa nitakayokuja kwako.