Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu The Tribe Of Naphtali

48 mistari · 26 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Bilha mtumishi wa kike wa Raheli akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa pili.

  2. Ndipo Raheli akasema, “Nilikuwa na mashindano makubwa na ndugu yangu, nami nimeshinda.” Kwa hiyo akamwita Naftali.

  3. “Naftali ni kulungu jike aliyeachiwa huru azaaye watoto wazuri.

  4. kutoka Naftali, ni Ahira mwana wa Enani.”

  5. Kutoka wazao wa Naftali: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

  6. Idadi kutoka kabila la Naftali walikuwa watu 53,400.

  7. Upande wa kaskazini kutakuwa na makundi ya kambi ya Dani, chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Dani ni Ahiezeri mwana wa Amishadai.

  8. Kabila la Naftali litafuata. Kiongozi wa watu wa Naftali ni Ahira mwana wa Enani.

  9. Siku ya kumi na mbili Ahira mwana wa Enani, kiongozi wa watu wa Naftali, alileta sadaka yake.

  10. Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

  11. sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

  12. fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

  13. mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

  14. maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Ahira mwana wa Enani.

  15. Mwishowe, kama kikosi cha nyuma cha ulinzi wa vikosi vyote, vikosi vya kambi ya Dani viliondoka chini ya alama yao. Ahiezeri mwana wa Amishadai alikuwa kiongozi wao.

  16. naye Ahira mwana wa Enani aliongoza kikosi cha kabila la Naftali.

  17. kutoka kabila la Naftali, Nabi mwana wa Wofsi;

  18. Wazao wa Naftali kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Yaseeli, ukoo wa Wayaseeli; kutoka kwa Guni, ukoo wa Waguni;

  19. kutoka kwa Yeseri, ukoo wa Wayeseri; kutoka kwa Shilemu, ukoo wa Washilemu.

  20. Hizi ndizo zilizokuwa koo za Naftali; wale waliohesabiwa walikuwa 45,400.

  21. Pedaheli mwana wa Amihudi, kiongozi kutoka kabila la Naftali.”

  22. Makabila haya yatasimama juu ya Mlima Ebali kwa kutamka laana: Reubeni, Gadi, Asheri, Zabuloni, Dani na Naftali.

  23. Kuhusu Naftali akasema: “Naftali amejaa tele upendeleo wa Bwana, naye amejaa baraka yake; atarithi magharibi na kusini.”

  24. Kura ya sita ikaangukia kabila la Naftali, ukoo kwa ukoo:

  25. Mpaka wao uliendelea kutoka Helefi na kwenye mti mkubwa ulio katika Saananimu, ukipitia Adami-Nekebu na Yabineeli hadi Lakumu, na kuishia katika Mto Yordani.