Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Thanksgiving: For the grace bestowed on others

8 mistari · 57 vipengele

Mistari kuhusu For the grace bestowed on others

  1. Ninamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu kwa sababu ya neema yake mliyopewa katika Kristo Yesu.

  2. Ninamshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo ninyi.

  3. Katika maombi yangu yote daima nimekuwa nikiwaombea ninyi nyote kwa furaha,

  4. kwa sababu ya kushiriki kwenu katika kueneza Injili, tangu siku ya kwanza hadi leo.

  5. Siku zote tunamshukuru Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, tunapowaombea ninyi,

  6. kwa sababu tumesikia kuhusu imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo wenu mlio nao kwa watakatifu wote:

  7. imani na upendo ule utokao katika tumaini mlilowekewa akiba mbinguni, na ambalo mmesikia habari zake katika neno la kweli, yaani, ile Injili

  8. iliyowafikia ninyi. Duniani kote Injili hii inazaa matunda na kuenea kama ilivyokuwa kwenu tangu siku ile mlipoisikia na kuielewa neema ya Mungu katika kweli yote.