Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Self-Examination

23 mistari · 9 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

  1. Ni makosa na dhambi ngapi nilizotenda? Nionyeshe kosa langu na dhambi yangu.

  2. Katika hasira yako, usitende dhambi. Mkiwa vitandani mwenu, mtulie kimya mkiichunguza mioyo yenu.

  3. Ni nani awezaye kutambua makosa yake? Nisamehe makosa yangu nisiyoyajua.

  4. Ee Bwana, unijaribu, unipime, uuchunguze moyo wangu na mawazo yangu;

  5. nilikumbuka nilivyoimba nyimbo usiku. Moyo wangu ulitafakari na roho yangu ikauliza:

  6. Nimezifikiri njia zangu na nimeelekeza hatua zangu katika mausia yako.

  7. Ee Mungu, nichunguze, uujue moyo wangu, nijaribu na ujue mawazo yangu.

  8. Uone kama kuna njia iletayo machukizo ndani yangu, uniongoze katika njia ya milele.

  9. Moyo ni mdanganyifu kuliko vitu vyote, ni mwovu kupita kiasi. Ni nani awezaye kuujua?

  10. Tuzichunguze njia zetu na kuzijaribu, na tumrudie Bwana Mungu.

  11. Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Zitafakarini vyema njia zenu.

  12. Wakahuzunika sana, wakaanza kumuuliza mmoja baada ya mwingine, “Je, ni mimi Bwana?”

  13. Wakaanza kuhuzunika na kumuuliza mmoja baada ya mwingine, “Je, ni mimi Bwana?”

  14. Kwa hiyo, mtu yeyote alaye mkate huo au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa na hatia ya dhambi juu ya mwili na damu ya Bwana.

  15. Inampasa mtu ajichunguze mwenyewe, kabla ya kula mkate na kukinywea kikombe.

  16. Lakini kama tungejichunguza wenyewe tusingehukumiwa.

  17. Jichunguzeni wenyewe mwone kama mnaishi katika imani. Jipimeni wenyewe. Je, hamtambui ya kuwa Yesu Kristo yumo ndani yenu? Kama sivyo, basi, mmeshindwa kufikia kipimo hicho!

  18. Kama mtu yeyote akijiona kuwa yeye ni bora na kumbe sivyo, basi mtu huyo anajidanganya mwenyewe.

  19. Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo aweze kujisifu, bila kujilinganisha na mtu mwingine.

  20. Kwa maana, kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe.

  21. kila mara mioyo yetu inapotuhukumu. Kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu, naye anajua kila kitu.

  22. Wapendwa, kama mioyo yetu haituhukumu, tunao ujasiri mbele za Mungu,

  23. lolote tuombalo, twalipokea kutoka kwake, kwa sababu tumezitii amri zake na kutenda yale yanayompendeza.