Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Rulers

255 mistari · 5 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Zaburi ya Solomoni. Ee Mungu, mjalie mfalme aamue kwa haki yako, mwana wa mfalme kwa haki yako.

  2. Atawaamua watu wako kwa haki, watu wako walioonewa kwa haki.

  3. Milima italeta mafanikio kwa watu, vilima tunda la haki.

  4. Atawatetea walioonewa miongoni mwa watu na atawaokoa watoto wa wahitaji, ataponda mdhalimu.

  5. Atadumu kama jua lidumuvyo, kama mwezi, vizazi vyote.

  6. Atakuwa kama mvua inyeshayo juu ya shamba lililofyekwa, kama manyunyu yanyeshayo ardhi.

  7. Katika siku zake wenye haki watastawi; mafanikio yatakuwepo mpaka mwezi utakapokoma.

  8. Atatawala kutoka bahari hadi bahari na kutoka Mto mpaka miisho ya dunia.

  9. Makabila ya jangwani watamsujudia, na adui zake wataramba mavumbi.

  10. Wafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbali watamletea kodi; wafalme wa Sheba na Seba watampa zawadi.

  11. Wafalme wote watamsujudia na mataifa yote yatamtumikia.

  12. Kwa maana atamwokoa mhitaji anayemlilia, aliyeonewa asiye na wa kumsaidia.

  13. Atawahurumia wanyonge na wahitaji na kuwaokoa wahitaji kutoka mauti.

  14. Atawaokoa kutoka uonevu na ukatili, kwani damu yao ni ya thamani machoni pake.

  15. Aishi maisha marefu! Na apewe dhahabu ya Sheba. Watu wamwombee daima na kumbariki mchana kutwa.

  16. Nafaka ijae tele katika nchi yote, juu ya vilele vya vilima na istawi. Tunda lake na listawi kama Lebanoni, listawi kama majani ya kondeni.

  17. Jina lake na lidumu milele, na lidumu kama jua. Mataifa yote yatabarikiwa kupitia kwake, nao watamwita aliyebarikiwa.

  18. “Hata lini utaendelea kuwatetea wasio haki na kuonyesha upendeleo kwa waovu?

  19. Teteeni wanyonge na yatima, tunzeni haki za maskini na walioonewa.

  20. Mwokoeni mnyonge na mhitaji, wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu.

  21. Je, kiti cha utawala wa udhalimu kitajiunga nawe, ule utawala uletao taabu kutokana na sheria zake?

  22. Huungana kuwashambulia wenye haki, kuwahukumu kufa wasio na hatia.

  23. Bwana yuko mkono wako wa kuume, atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake.

  24. wafalme wa dunia na mataifa yote, ninyi wakuu na watawala wote wa dunia,

  25. Wote na walisifu jina la Bwana, kwa maana jina lake pekee limetukuka, utukufu wake uko juu ya nchi na mbingu.