Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Rulers: Character and qualifications of

77 mistari · 5 vipengele

Mistari kuhusu Character and qualifications of

Chuja kwa kitabu
  1. “Basi sasa Farao na atafute mtu mwenye akili na hekima ili amweke kuwa msimamizi wa nchi ya Misri.

  2. Lakini uchague watu wenye uwezo miongoni mwa watu wote, watu wanaomwogopa Mungu, watu waaminifu wanaochukia mali ya dhuluma, uwateuwe wawe maafisa juu ya maelfu, mamia, hamsini na makumi.

  3. Waweke wawe waamuzi wa watu kwa wakati wote, lakini waambie wakuletee kila shauri lililo gumu; yale yaliyo rahisi wayaamue wao wenyewe. Hii itafanya mzigo wako kuwa mwepesi, kwa sababu watashirikiana nawe.

  4. “Usipokee rushwa, kwa kuwa rushwa hupofusha wale waonao, na kupinda maneno ya wenye haki.

  5. Chagueni baadhi ya watu wenye hekima, wenye ufahamu na wanaoheshimika kutoka kila kabila lenu, nami nitawaweka juu yenu.”

  6. Wateue waamuzi na maafisa kwa kila kabila lenu katika kila mji ambao Bwana Mungu wenu anawapa, nao watawaamua watu kwa usawa.

  7. Msipotoshe haki wala msifanye upendeleo. Msikubali rushwa kwa sababu rushwa hupofusha macho ya wenye busara na kugeuza maneno ya wenye haki.

  8. Mfuate haki na haki peke yake, ili mweze kuishi na kuimiliki nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa.

  9. “Alaaniwe mtu apotoshaye haki ya mgeni, yatima au mjane.”

  10. Mungu wa Israeli alinena, mwamba wa Israeli akaniambia: ‘Mtu anatawala watu kwa haki, wakati anapotawala akiwa na hofu ya Mungu,

  11. yeye ni kama mwanga wa asubuhi jua lichomozapo asubuhi isiyo na mawingu, kama mwanga baada ya mvua uchipuzao majani kutoka ardhini.’

  12. Nawe Ezra, kufuatana na hekima ya Mungu wenu uliyo nayo, weka mahakimu na waamuzi wote wanaozifahamu sheria za Mungu wenu ili watoe haki kwa watu wote wa Ngʼambo ya Mto Frati. Nawe inakupasa umfundishe yeyote ambaye hazifahamu.

  13. Kwa hiyo, ninyi wafalme, kuweni na hekima; mwonyeke, enyi watawala wa dunia.

  14. Mtumikieni Bwana kwa hofu na mshangilie kwa kutetemeka.

  15. Zaburi ya Solomoni. Ee Mungu, mjalie mfalme aamue kwa haki yako, mwana wa mfalme kwa haki yako.

  16. Atawaamua watu wako kwa haki, watu wako walioonewa kwa haki.

  17. Milima italeta mafanikio kwa watu, vilima tunda la haki.

  18. Atawatetea walioonewa miongoni mwa watu na atawaokoa watoto wa wahitaji, ataponda mdhalimu.

  19. Atadumu kama jua lidumuvyo, kama mwezi, vizazi vyote.

  20. Atakuwa kama mvua inyeshayo juu ya shamba lililofyekwa, kama manyunyu yanyeshayo ardhi.

  21. Katika siku zake wenye haki watastawi; mafanikio yatakuwepo mpaka mwezi utakapokoma.

  22. Atatawala kutoka bahari hadi bahari na kutoka Mto mpaka miisho ya dunia.

  23. Makabila ya jangwani watamsujudia, na adui zake wataramba mavumbi.

  24. Wafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbali watamletea kodi; wafalme wa Sheba na Seba watampa zawadi.

  25. Wafalme wote watamsujudia na mataifa yote yatamtumikia.