Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Retaliation

38 mistari · 1 kipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Lakini kukiwa na jeraha kubwa, ni lazima ulipe uhai kwa uhai,

  2. jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu,

  3. kuchomwa moto kwa kuchomwa moto, jeraha kwa jeraha, mchubuko kwa mchubuko.

  4. “ ‘Usijilipizie kisasi wala kuwa na kinyongo dhidi ya mmoja wa jamaa yako, lakini mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Mimi ndimi Bwana.

  5. “ ‘Kama mtu yeyote atamuua mtu mwingine, ni lazima auawe.

  6. Mtu yeyote auaye mnyama wa mtu mwingine lazima afidie, uhai kwa uhai.

  7. Ikiwa mtu yeyote atamjeruhi jirani yake, chochote alichomtenda naye atatendewa:

  8. iwapo amemvunja mfupa atavunjwa mfupa, jicho kwa jicho, jino kwa jino. Kama alivyomjeruhi mwenzake, vivyo hivyo ndivyo atakavyojeruhiwa.

  9. Yeyote auaye mnyama wa mtu lazima alipe fidia, lakini yeyote auaye mtu, lazima auawe.

  10. Mtakuwa na sheria iyo hiyo kwa mgeni na kwa mzawa. Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.’ ”

  11. basi mtende kama alivyotaka kumtendea ndugu yake. Ni lazima mwondoe uovu miongoni mwenu.

  12. Watu watakaosalia watasikia hili na kuogopa, uovu kama huo kamwe hautatendeka tena miongoni mwenu.

  13. Msionyeshe huruma, uhai kwa uhai, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu.

  14. Katika kiburi chake, mwovu humtesa maskini, waovu na wanaswe katika hila wanazozitunga.

  15. Usiseme, “Nitakulipiza kwa ajili ya kosa hili!” Mngojee Bwana, naye atakuokoa.

  16. Usiseme, “Nitamtenda kama alivyonitenda mimi; nitamlipiza mtu yule kwa kile alichonitendea.”

  17. Kama mtu akichimba shimo, atatumbukia ndani yake, kama mtu akivingirisha jiwe, litamrudia.

  18. Ole wako wewe, ee mharabu, wewe ambaye hukuharibiwa! Ole wako, ee msaliti, wewe ambaye hukusalitiwa! Utakapokwisha kuharibu, utaharibiwa; utakapokwisha kusaliti, utasalitiwa.

  19. “Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Jicho kwa jicho na jino kwa jino.’

  20. Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu. Lakini kama mtu akikupiga kwenye shavu la kuume, mgeuzie na la pili pia.

  21. Kama mtu akitaka kukushtaki na kuchukua joho lako, mwachie achukue na koti pia.

  22. Kama mtu akikulazimisha kwenda maili moja, nenda naye maili mbili.

  23. Mpe yeye akuombaye, wala usimgeuzie kisogo yeye atakaye kukukopa.

  24. “Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Mpende jirani yako na umchukie adui yako.’

  25. Lakini ninawaambia: Wapendeni adui zenu na waombeeni wanaowatesa ninyi,