Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Regeneration: General references

256 mistari · 1 kipengele

Mistari kuhusu General references

Chuja kwa kitabu
  1. Lakini mpaka leo Bwana hajawapa akili ya kuelewa au macho yanayoona au masikio yanayosikia.

  2. Bwana Mungu wako ataitahiri mioyo yenu na mioyo ya wazao wenu ili mweze kumpenda kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote ukaishi.

  3. Yeye na aielekeze mioyo yetu kwake, ili tutembee katika njia zake zote na kuzishika amri na maagizo na masharti aliyowapa baba zetu.

  4. Kuwa pamoja nawe ni kijito cha uzima, katika nuru yako twaona nuru.

  5. Unioshe na uovu wangu wote na unitakase dhambi yangu.

  6. Nioshe kwa hisopo, nami nitakuwa safi, unisafishe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.

  7. Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu.

  8. Tulipokuwa tumefunikwa kabisa na dhambi, wewe ulisamehe makosa yetu.

  9. Ulipopanda juu, uliteka mateka, ukapokea vipawa kutoka kwa wanadamu, hata kutoka kwa wale walioasi, ili wewe, Ee Bwana Mungu, upate kuishi huko.

  10. “Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu na Babeli miongoni mwa wale wanaonikubali mimi: Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi, nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ”

  11. Bwana ataandika katika orodha ya mataifa: “Huyu alizaliwa Sayuni.”

  12. Askari wako watajitolea kwa hiari katika siku yako ya vita. Ukiwa umevikwa fahari takatifu, kutoka tumbo la mapambazuko utapokea umande wa ujana wako.

  13. Zaidi ya yote, linda moyo wako, kuliko yote uyalindayo, maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

  14. Katika njia ya haki kuna uzima; katika mapito hayo kuna maisha ya milele.

  15. Kumcha Bwana ni chemchemi ya uzima, ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti.

  16. Mipango ya moyoni ni ya mwanadamu, bali jibu la ulimi hutoka kwa Bwana.

  17. jiosheni na mkajitakase. Yaondoeni matendo yenu maovu mbele zangu! Acheni kutenda mabaya,

  18. jifunzeni kutenda mema! Tafuteni haki, watieni moyo walioonewa. Teteeni shauri la yatima, wateteeni wajane.

  19. Nitauelekeza mkono wangu dhidi yenu, nitawasafisha takataka zenu zote na kuwaondolea unajisi wenu wote.

  20. Bwana atausafisha uchafu wa wanawake wa Sayuni, atatakasa madoa ya damu kutoka Yerusalemu kwa Roho ya hukumu na Roho ya moto.

  21. Kwa furaha mtachota maji kutoka visima vya wokovu.

  22. Bwana, unaamuru amani kwa ajili yetu, yale yote tuliyoweza kuyakamilisha ni wewe uliyetenda kwa ajili yetu.

  23. Wakati watakapoona watoto wao miongoni mwao, kazi ya mikono yangu, watalitakasa Jina langu takatifu; wataukubali utakatifu wa yeye Aliye Mtakatifu wa Yakobo, nao watamcha Mungu wa Israeli.

  24. Ndipo macho ya wale wanaoona hayatafumbwa tena, nayo masikio ya wale wanaosikia yatasikiliza.

  25. Moyo wa mtu mwenye hamaki utafahamu na kuelewa, nao ulimi wenye kigugumizi utanena kwa ufasaha.