Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Patience: General references

60 mistari · 37 vipengele

Mistari kuhusu General references

Chuja kwa kitabu
  1. Tulia mbele za Bwana na umngojee kwa uvumilivu; usisumbuke watu wanapofanikiwa katika njia zao, wanapotekeleza mipango yao miovu.

  2. Epuka hasira na uache ghadhabu, usihangaike: itakuongoza tu kutenda uovu.

  3. Kwa maana waovu watakatiliwa mbali, bali wale wanaomtumaini Bwana watairithi nchi.

  4. Mtu mwepesi wa hasira huchochea ugomvi, bali mtu mvumilivu hutuliza ugomvi.

  5. Mwisho wa jambo ni bora kuliko mwanzo wake, uvumilivu ni bora kuliko kiburi.

  6. Usiwe mwepesi kukasirika rohoni mwako, kwa kuwa hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.

  7. ni vyema kungojea kwa utulivu kwa ajili ya wokovu wa Bwana.

  8. Ni vyema mtu kuchukua nira bado angali kijana.

  9. Lakini zile mbegu zilizoanguka kwenye udongo mzuri ni mfano wa wale ambao hulisikia neno la Mungu na kulishika kwa moyo mnyofu wa utiifu, nao kwa kuvumilia kwingi huzaa matunda.

  10. Kwa kuvumilia mtaokoa roho zenu.

  11. Wale ambao kwa kuvumilia katika kutenda mema hutafuta utukufu, heshima na maisha yasiyoharibika, Mungu atawapa uzima wa milele.

  12. Si hivyo tu, bali twafurahi pia katika mateso, kwa sababu tunajua kuwa mateso huleta saburi,

  13. nayo saburi huleta uthabiti wa moyo, na uthabiti wa moyo huleta tumaini,

  14. Lakini tunapotumaini kupata kitu ambacho hatuna, basi twakingojea kwa saburi.

  15. Kuweni na furaha katika tumaini, katika dhiki kuweni na saburi, dumuni katika maombi.

  16. Kwa maana kila kitu kilichoandikwa zamani, kiliandikwa kutufundisha, ili kwamba kwa saburi na faraja tunayopata katika Maandiko tuwe na tumaini.

  17. Mungu atoaye saburi na faraja, awajalie ninyi roho ya umoja miongoni mwenu mnapomfuata Kristo Yesu,

  18. Upendo huvumilia, upendo hufadhili, upendo hauoni wivu, hauna majivuno, hauna kiburi.

  19. Haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, haukasiriki upesi, hauweki kumbukumbu ya mabaya.

  20. Bali kama watumishi wa Mungu tuonyeshe kwa kila njia: katika saburi nyingi; katika dhiki, katika misiba, na katika shida;

  21. katika kupigwa, katika kufungwa gerezani na katika ghasia; katika kazi ngumu, katika kukesha na katika kufunga;

  22. katika utakatifu, katika ufahamu, katika uvumilivu, na katika utu wema; katika Roho Mtakatifu na upendo wa kweli;

  23. Mambo yanayomtambulisha mtume wa kweli, yaani, ishara, miujiza na maajabu, yalifanywa miongoni mwenu kwa saburi nyingi.

  24. Hivyo, tusichoke katika kutenda mema, kwa kuwa tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa.

  25. Basi, mimi niliye mfungwa wa Bwana, nawasihi mwenende kama inavyostahili wito wenu mlioitiwa.