Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Moabites: Possessed many and great cities

10 mistari · 56 vipengele

Mistari kuhusu Possessed many and great cities

  1. “Moto uliwaka kutoka Heshboni, mwali wa moto kutoka mji wa Sihoni. Uliteketeza Ari ya Moabu, raiya wa mahali pa Arnoni palipoinuka.

  2. “Lakini tumewashinda; Heshboni umeharibiwa hadi Diboni. Tumebomoa hadi kufikia Nofa, ulioenea hadi Medeba.”

  3. Neno kuhusu Moabu: Ari iliyo Moabu imeangamizwa: imeharibiwa kwa usiku mmoja! Kiri iliyo Moabu imeangamizwa, imeharibiwa kwa usiku mmoja!

  4. Diboni anakwea hadi kwenye hekalu lake, mpaka mahali pake pa juu ili walie, Moabu anaombolezea Nebo na Medeba. Kila kichwa kimenyolewa na kila ndevu limeondolewa.

  5. Wamevaa nguo za magunia barabarani, juu ya mapaa na kwenye viwanja wote wanaomboleza, wamelala kifudifudi kwa kulia.

  6. Heshboni na Eleale wanalia, sauti zao zinasikika hadi Yahazi. Kwa hiyo watu wenye silaha wa Moabu wanapiga kelele, nayo mioyo yao imezimia.

  7. Hukumu imefika kwenye uwanda wa juu: katika Holoni, Yahasa na Mefaathi,

  8. katika Diboni, Nebo na Beth-Diblathaimu,

  9. katika Kiriathaimu, Beth-Gamuli na Beth-Meoni,

  10. katika Keriothi na Bosra; kwa miji yote ya Moabu, iliyoko mbali na karibu.