Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Meteorology and Celestial Phenomena: General references

150 mistari · 2 vipengele

Mistari kuhusu General references

Chuja kwa kitabu
  1. hapakuwepo na mche wa shambani uliokuwa umejitokeza ardhini, wala hapakuwepo na mmea wa shamba uliokuwa umeota, kwa kuwa Bwana Mungu alikuwa hajanyeshea mvua juu ya nchi, na hapakuwepo mtu wa kuilima ardhi,

  2. lakini umande ulitokeza kutoka ardhini na kunyesha uso wote wa nchi:

  3. Baba yake Isaki akamjibu, akamwambia, “Makao yako yatakuwa mbali na utajiri wa dunia, mbali na umande wa mbinguni juu.

  4. Husema na jua, nalo likaacha kuangaza; naye huizima mianga ya nyota.

  5. Hutandaza anga la kaskazini mahali patupu; naye huiningʼiniza dunia mahali pasipo na kitu.

  6. Huyafungia maji kwenye mawingu yake, hata hivyo mawingu hayapasuki kwa uzito wake.

  7. Nguzo za mbingu nazo zatetemeka, zinatishika anapozikemea.

  8. Vitisho humjia kama mafuriko; dhoruba humkumba ghafula usiku.

  9. Upepo mkali wa mashariki humchukua, naye hutoweka; humzoa kutoka mahali pake.

  10. kwa maana yeye huitazama miisho ya dunia na huona kila kitu chini ya mbingu.

  11. Alipofanyiza nguvu za upepo na kuyapima maji,

  12. alipofanya maagizo kwa ajili ya mvua na njia kwa ajili ya umeme wa radi,

  13. ndipo alipoitazama hekima na kuikadiria thamani yake, akaithibitisha na kuihakikisha.

  14. Mizizi yangu itafika mpaka kwenye maji, nao umande utakaa juu ya matawi yangu usiku kucha.

  15. “Yeye huvuta juu matone ya maji, ayachujayo kama mvua kutoka kwenye vijito;

  16. mawingu huangusha chini maji yake, nayo mvua nyingi huwanyeshea wanadamu.

  17. Ni nani ajuaye jinsi ayatandazavyo mawingu, jinsi angurumavyo kutoka hemani mwake.

  18. Tazama jinsi anavyotandaza umeme wa radi kumzunguka, naye huvifunika vilindi vya bahari.

  19. Hivi ndivyo atawalavyo mataifa, na kuwapa chakula kwa wingi.

  20. Huujaza mkono wake kwa umeme wa radi, na kuuagiza kulenga shabaha yake.

  21. Ngurumo zake hutangaza dhoruba inayokuja; hata mifugo hujulisha kukaribia kwake.

  22. Huiambia theluji, ‘Anguka juu ya dunia,’ nayo manyunyu ya mvua, ‘Uwe mvua ya nguvu.’

  23. Ili wanadamu wote aliowaumba wapate kujua kazi zake, yeye humzuilia kila mtu shughuli zake.

  24. Wanyama hujificha; hubakia kwenye mapango yao.

  25. Dhoruba hutoka katika chumba chake, baridi hutoka katika upepo uendao kasi.