Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Mariner

36 mistari · 3 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Wengine walisafiri baharini kwa meli, walikuwa wafanyabiashara kwenye maji makuu.

  2. Waliziona kazi za Bwana, matendo yake ya ajabu kilindini.

  3. Kwa maana alisema na kuamsha tufani iliyoinua mawimbi juu.

  4. Yakainuka juu mbinguni, yakashuka chini hadi vilindini, katika hatari hii ujasiri wao uliyeyuka.

  5. Walipepesuka na kuyumbayumba kama walevi, ujanja wao ukafikia ukomo.

  6. Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawatoa kwenye taabu yao.

  7. Akatuliza dhoruba kwa mnongʼono, mawimbi ya bahari yakatulia.

  8. Walifurahi ilipokuwa shwari, naye akawaongoza hadi bandari waliyoitamani.

  9. Watu walipokwisha kuivuta mashua hiyo na kuiingiza katika meli, waliifunga kwa kamba chini ya meli yenyewe ili kuzishikanisha pamoja. Wakiogopa kupelekwa kwenye mchanga karibu na pwani ya Sirti, wakashusha matanga wakaiacha meli isukumwe na huo upepo.

  10. Tulikuwa tunapigwa na dhoruba kwa nguvu, kiasi kwamba kesho yake walianza kutupa shehena toka melini.

  11. Siku ya tatu, wakatupa vyombo vya meli baharini kwa mikono yao wenyewe.

  12. Kulipokuwa hakuna kuonekana kwa jua wala nyota kwa siku nyingi, nayo dhoruba ikiwa inaendelea kuwa kali, hatimaye tulikata kabisa tamaa ya kuokoka.

  13. Baada ya watu kukaa siku nyingi bila kula chakula, Paulo akasimama katikati yao akasema, “Enyi watu, iliwapasa kunisikiliza na kuacha kusafiri baharini kutoka Krete, ndipo ninyi mngekuwa mmejinusuru na uharibifu huu na hasara hii.

  14. Sasa ninawasihi sana, jipeni moyo mkuu kwa kuwa hakuna hata mmoja wenu atakayepoteza maisha yake, ila meli itaangamia.

  15. Jana usiku, malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni wake na ambaye ninamwabudu alisimama karibu nami,

  16. naye akasema, ‘Paulo usiogope, kwa kuwa ni lazima usimame mbele ya Kaisari, naye Mungu amekupa kwa neema uhai wa wote wanaosafiri pamoja nawe.

  17. Hivyo jipeni moyo, enyi watu, kwa kuwa ninamwamini Mungu kwamba yatakuwa kama vile alivyoniambia.’

  18. Lakini hata hivyo meli yetu itakwama kwenye kisiwa fulani.”

  19. Usiku wa kumi na nne ulipofika, tulikuwa bado tunasukumwa na upepo katika Bahari ya Adria. Ilipokuwa yapata usiku wa manane, mabaharia wakahisi kwamba walikuwa wanakaribia nchi kavu.

  20. Kwa hiyo wakapima kina cha maji na kukuta kilikuwa pima ishirini, baada ya kuendelea mbele kidogo wakapima tena wakapata kina cha pima kumi na tano.

  21. Wakiogopa kwamba meli yetu ingegonga kwenye miamba, wakashusha nanga nne za nyuma ya meli, wakawa wanaomba kupambazuke.

  22. Katika jaribio la kutoroka kutoka kwenye meli, mabaharia wakashusha mashua ya kuokolea watu baharini, wakijifanya kwamba wanakwenda kushusha nanga za omo.

  23. Ndipo Paulo akamwambia yule jemadari na askari, “Hawa watu wasipobaki katika meli, hamtaweza kuokoka.”

  24. Hivyo basi wale askari wakakata kamba zilizoshikilia ile mashua ya kuokolea watu kwenye meli, wakaiacha ianguke humo baharini.

  25. Kabla ya mapambazuko, Paulo akawasihi watu wote wale chakula akisema, “Leo ni siku ya kumi na nne mmekuwa katika wasiwasi mkiwa mmefunga na bila kula chochote.