Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Jacob

285 mistari · 49 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi, watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu namna hii, ndio Baba anawatafuta.

  2. Mungu ni Roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”

  3. Yule mwanamke akamwambia, “Ninafahamu kwamba Masiya (aitwaye Kristo) anakuja. Yeye akija, atatueleza mambo yote.”

  4. Yesu akamwambia, “Mimi ninayezungumza nawe, ndiye.”

  5. Wakati huo wanafunzi wake wakarudi, wakashangaa sana kumwona akizungumza na mwanamke. Lakini hakuna aliyemuuliza, “Unataka nini kwake?” Au “Kwa nini unazungumza naye?”

  6. Yule mwanamke akaacha mtungi wake, akarudi mjini akawaambia watu,

  7. “Njooni mkamwone mtu aliyeniambia kila kitu nilichotenda! Je, yawezekana huyu ndiye Kristo?”

  8. Basi wakamiminika watu kutoka mjini wakamwendea Yesu.

  9. Ndipo Yosefu akawatuma kumleta Yakobo baba yake pamoja na jamaa yake yote, jumla yao walikuwa watu sabini na watano.

  10. Hivyo Yakobo akaenda Misri ambako yeye na baba zetu walifia.