Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Industry: General references

39 mistari · 23 vipengele

Mistari kuhusu General references

Chuja kwa kitabu
  1. Mikono mivivu hufanya mtu kuwa maskini lakini mikono yenye bidii huleta utajiri.

  2. Yeye akusanyaye mazao wakati wa kiangazi ni mwana mwenye hekima, lakini yeye alalaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha.

  3. Hakikisha kuwa unajua hali ya makundi yako ya kondoo na mbuzi, angalia kwa bidii ngʼombe zako.

  4. Kwa kuwa utajiri haudumu milele, nayo taji haidumu vizazi vyote.

  5. Wakati majani makavu yameondolewa na mapya yamechipua, nayo majani toka milimani yamekusanywa,

  6. wana-kondoo watakupatia mavazi na mbuzi thamani ya shamba.

  7. Utakuwa na maziwa mengi ya mbuzi kukulisha wewe na jamaa yako, na kuwalisha watumishi wako wa kike.

  8. Mchwa ni viumbe wenye nguvu ndogo, hata hivyo hujiwekea akiba ya chakula chao wakati wa kiangazi.

  9. Pelele ni viumbe vyenye uwezo mdogo hata hivyo hujitengenezea nyumba zao kwenye miamba.

  10. Nzige hawana mfalme, hata hivyo huenda pamoja vikosi vikosi.

  11. Mjusi anaweza kushikwa kwa mkono, hata hivyo huonekana katika majumba ya kifalme.

  12. Huchagua sufu na kitani naye hufanya kazi kwa mikono yenye bidii.

  13. Yeye ni kama meli za biashara akileta chakula chake kutoka mbali.

  14. Yeye huamka kungali bado giza huwapa jamaa yake chakula na mafungu kwa watumishi wake wa kike.

  15. Huangalia shamba na kulinunua, kutokana na mapato yake hupanda shamba la mizabibu.

  16. Hufanya kazi zake kwa nguvu, mikono yake ina nguvu kwa ajili ya kazi zake.

  17. Huona kwamba biashara yake ina faida, wala taa yake haizimiki usiku.

  18. Huweka mikono yake kwenye pia, navyo vidole vyake hushikilia kijiti chenye uzi.

  19. Huwanyooshea maskini mikono yake na kuwakunjulia wahitaji vitanga vyake.

  20. Theluji ishukapo, hana hofu kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake, kwa maana wote wamevikwa nguo za kutia joto.

  21. Hutengeneza mazulia ya urembo ya kufunika kitanda chake, yeye huvaa kitani safi na urujuani.

  22. Mume wake anaheshimiwa kwenye lango la mji, aketipo miongoni mwa wazee wa nchi.

  23. Hutengeneza mavazi ya kitani na kuyauza, naye huwauzia wafanyabiashara mishipi.

  24. Amevikwa nguvu na heshima, anaweza kucheka bila kuwa na hofu kwa siku zijazo.

  25. Huzungumza kwa hekima na mafundisho ya kuaminika yapo ulimini mwake.