Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Gershon

21 mistari · 1 kipengele

Mistari muhimu ya Biblia

  1. Haya ndiyo majina ya wana wa Lawi kufuatana na orodha zao: Gershoni, Kohathi na Merari. Lawi aliishi miaka 137.

  2. Wana wa Gershoni kwa koo, walikuwa Libni na Shimei.

  3. Haya yalikuwa majina ya wana wa Lawi: Gershoni, Kohathi na Merari.

  4. Haya ndiyo yaliyokuwa majina ya koo za Wagershoni: Libni na Shimei.

  5. Koo za Wakohathi zilikuwa ni: Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.

  6. Koo za Wamerari zilikuwa ni: Mahli na Mushi. Hizi ndizo zilizokuwa koo za Walawi, kufuatana na jamaa zao.

  7. Kulikuwa na koo za Walibni na Washimei kwa Gershoni; hizi ndizo zilizokuwa koo za Wagershoni.

  8. Idadi ya waume wote waliokuwa na mwezi mmoja au zaidi waliohesabiwa walikuwa 7,500.

  9. Ukoo wa Wagershoni walitakiwa kuweka kambi zao upande wa magharibi, nyuma ya Maskani.

  10. Kiongozi wa jamaa za Wagershoni alikuwa Eliasafu mwana wa Laeli.

  11. Katika Hema la Kukutania, Wagershoni walikuwa na wajibu wa kutunza Maskani na hema, vifuniko vyake, pazia katika mlango wa kuingilia ndani ya Hema la Kukutania,

  12. mapazia ya ua, pazia katika ingilio la ua unaozunguka Maskani na madhabahu, pamoja na kamba, na kila kinachohusika kwa matumizi yake.

  13. “Wahesabu pia Wagershoni kwa jamaa zao na koo zao.

  14. Wahesabu wanaume wote wenye umri wa miaka thelathini hadi hamsini ambao huja kutumika katika Hema la Kukutania.

  15. “Hii ndiyo huduma ya koo za Wagershoni wakati wanapofanya kazi na kubeba mizigo.

  16. Watabeba mapazia ya maskani. Hema la Kukutania, kifuniko chake na kifuniko cha nje cha ngozi za pomboo, mapazia ya maingilio ya Hema la Kukutania,

  17. mapazia ya ua unaozunguka Maskani na madhabahu, pazia la maingilio, kamba na vifaa vyote vinavyotumika katika huduma yake. Wagershoni watafanya yote yatakiwayo kufanyika na vitu hivi.

  18. Utumishi wao wote ukiwa ni kuchukua au wa kufanya kazi nyingine, utafanyika chini ya maelekezo ya Aroni na wanawe. Mtawapangia kama wajibu wao yote watakayoyafanya.

  19. Hii ndiyo huduma ya koo za Wagershoni katika Hema la Kukutania. Wajibu wao utakuwa chini ya maelekezo ya Ithamari mwana wa kuhani Aroni.

  20. Wana wa Lawi walikuwa: Gershoni, Kohathi na Merari.

  21. Haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni: Libni na Shimei.