Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Egypt

328 mistari · 105 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Wale watakaonusurika upanga na kurudi katika nchi ya Yuda kutoka Misri watakuwa wachache sana. Ndipo mabaki wote wa Yuda waliokuja kuishi Misri watakapojua ni neno la nani litakalosimama, kwamba ni langu au lao.

  2. Kuhusu Misri: Huu ni ujumbe dhidi ya jeshi la Farao Neko mfalme wa Misri, lililoshindwa huko Karkemishi kwenye Mto Frati na Nebukadneza mfalme wa Babeli, katika mwaka wa nne wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda:

  3. “Wekeni tayari ngao zenu, kubwa na ndogo, mtoke kwa ajili ya vita!

  4. Fungieni farasi lijamu, pandeni farasi! Shikeni nafasi zenu mkiwa mmevaa chapeo! Isugueni mikuki yenu, vaeni dirii vifuani!

  5. Je, ninaona nini? Wametiwa hofu, wanarudi nyuma, askari wao wameshindwa. Wanakimbia kwa haraka pasipo kutazama nyuma, tena kuna hofu kuu kila upande,” asema Bwana.

  6. Walio wepesi na wenye mbio hawawezi kukimbia, wala wenye nguvu hawawezi kutoroka. Kaskazini, kando ya Mto Frati, wanajikwaa na kuanguka.

  7. “Ni nani huyu ajiinuaye kama Mto Naili, kama mito yenye maji yanayofanya mawimbi?

  8. Misri hujiinua kama Mto Naili, kama mito yenye maji yanayofanya mawimbi. Husema, ‘Nitainuka na kufunika dunia, nitaiangamiza miji na watu wake.’

  9. Songeni mbele, enyi farasi! Endesheni kwa ukali, enyi magari ya farasi, Endeleeni mbele, enyi mashujaa: watu wa Kushi na Putu wachukuao ngao, watu wa Ludi wavutao upinde.

  10. Lakini ile siku ni ya Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, siku ya kulipiza kisasi, kisasi juu ya adui zake. Upanga utakula hata utakapotosheka, hadi utakapozima kiu yake kwa damu. Kwa maana Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, atatoa dhabihu kwenye nchi ya kaskazini, kando ya Mto Frati.

  11. “Panda hadi Gileadi ukapate zeri, ee Bikira Binti wa Misri. Lakini umetumia dawa nyingi bila mafanikio; huwezi kupona.

  12. Mataifa yatasikia juu ya aibu yako, kilio chako kitaijaza dunia. Shujaa mmoja atajikwaa juu ya mwingine, nao wataanguka chini pamoja.”

  13. “ ‘Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitaleta upanga juu yako na kuua watu wako na wanyama wao.

  14. Misri itakuwa ukiwa na isiyolimwa wala kukaliwa na watu. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana. “ ‘Kwa sababu ulisema, “Mto Naili ni wangu; mimi niliufanya,”

  15. kwa hiyo mimi ni kinyume nawe na kinyume na vijito vyako, nami nitaifanya nchi ya Misri kuwa magofu na ukiwa isiyolimwa wala kukaliwa na watu kuanzia Migdoli hadi Aswani, hata kufikia mpakani wa Ethiopia.

  16. Hakuna unyayo wa mtu au mnyama utakaopita ndani yake, wala hakuna yeyote atakayeishi humo kwa muda wa miaka arobaini.

  17. Nitaifanya nchi ya Misri ukiwa, miongoni mwa nchi zilizo ukiwa, nayo miji yake itabaki ukiwa miaka arobaini miongoni mwa miji iliyo magofu. Nami nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huku na huko katika nchi nyingine.

  18. “Mwanadamu, Nebukadneza mfalme wa Babeli aliongoza jeshi lake kufanya kazi ngumu dhidi ya Tiro; kila kichwa kilipata upaa na kila bega likachunika. Lakini yeye na jeshi lake hawakupata malipo yoyote kutokana na muda wote aliongoza hiyo vita dhidi ya Tiro.

  19. Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitaitia Misri mikononi mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli, naye atachukua utajiri wa Misri. Atateka mateka na kuchukua nyara mali za Misri kama ujira kwa ajili ya jeshi lake.

  20. Nimempa mfalme wa Babeli nchi ya Misri kuwa ujira kwa juhudi zake kwa sababu yeye na jeshi lake walifanya kwa ajili yangu, asema Bwana Mwenyezi.

  21. Nitaifanya Pathrosi kuwa ukiwa na kuitia moto Soani, nami nitaipiga kwa adhabu Thebesi

  22. Nitaimwaga ghadhabu yangu juu ya Pelusiumu, ngome ya Misri, nami nitakatilia mbali makundi ya wajeuri wa Thebesi.

  23. Nitaitia moto nchi ya Misri; Pelusiumu itagaagaa kwa maumivu makuu. Thebesi itachukuliwa na tufani, Memfisi itakuwa katika taabu daima.

  24. Wanaume vijana wa Oni na wa Pi-Besethi wataanguka kwa upanga nayo hiyo miji itatekwa.

  25. Huko Tahpanhesi mchana utatiwa giza nitakapovunja kongwa la Misri; hapo kiburi cha nguvu zake kitakoma. Atafunikwa na mawingu na vijiji vyake vitatekwa.