Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Bartimeus: A blind man.

22 mistari · 1 kipengele

Mistari kuhusu A blind man.

  1. Yesu na wanafunzi wake walipokuwa wakiondoka Yeriko, umati mkubwa wa watu ulimfuata.

  2. Vipofu wawili walikuwa wameketi kando ya barabara. Waliposikia kwamba Yesu alikuwa anapita, wakapiga kelele wakisema, “Bwana, Mwana wa Daudi, tuhurumie!”

  3. Ule umati wa watu ukawakemea na kuwaambia wanyamaze, lakini wao wakazidi kupaza sauti, wakisema, “Bwana, Mwana wa Daudi, tuhurumie.”

  4. Yesu akasimama na kuwaita, akawauliza, “Mnataka niwafanyie nini?”

  5. Wakamjibu, “Bwana, tunataka kuona.”

  6. Yesu akawahurumia na kuwagusa macho yao. Mara macho yao yakapata kuona, nao wakamfuata.

  7. Kisha wakafika Yeriko. Yesu alipokuwa akiondoka mjini na wanafunzi wake pamoja na umati mkubwa wa watu, kipofu mmoja, jina lake Bartimayo, mwana wa Timayo, alikuwa ameketi kando ya njia akiomba msaada.

  8. Aliposikia kuwa ni Yesu wa Nazareti aliyekuwa anapita, akaanza kupaza sauti akisema, “Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!”

  9. Watu wengi wakamkemea, wakamwambia akae kimya, lakini yeye akazidi kupaza sauti, akisema, “Mwana wa Daudi, nihurumie!”

  10. Yesu akasimama na kusema, “Mwiteni.” Hivyo wakamwita yule mtu kipofu, wakamwambia, “Jipe moyo! Inuka, anakuita.”

  11. Akiwa analivua lile joho lake, alisimama na kumwendea Yesu.

  12. Yesu akamuuliza, “Unataka nikufanyie nini?” Yule kipofu akajibu, “Mwalimu, nataka kuona.”

  13. Yesu akamwambia, “Nenda zako, imani yako imekuponya.” Mara akapata kuona, akamfuata Yesu njiani.

  14. Yesu alipokuwa anakaribia Yeriko, kipofu mmoja alikuwa ameketi kando ya njia akiomba msaada.

  15. Kipofu huyo aliposikia umati wa watu ukipita, akauliza, “Kuna nini?”

  16. Wakamwambia, “Yesu wa Nazareti anapita.”

  17. Akapaza sauti, akasema, “Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!”

  18. Wale waliokuwa wametangulia mbele wakamkemea, wakamwambia akae kimya. Lakini yeye akapaza sauti zaidi, “Mwana wa Daudi, nihurumie!”

  19. Yesu akasimama, akawaamuru wamlete huyo mtu kwake. Alipokaribia, Yesu akamuuliza,

  20. “Unataka nikufanyie nini?” Akajibu, “Bwana, nataka kuona.”

  21. Yesu akamwambia, “Basi upate kuona. Imani yako imekuponya.”

  22. Akapata kuona saa ile ile, akamfuata Yesu, huku akimsifu Mungu. Watu wote walipoona mambo hayo, nao wakamsifu Mungu.