circa 6 BC – AD 30
The Life of Jesus
The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.
Mistari ya kipindi hiki
- Mathayo 18:18takriban 32 BK
“Amin, nawaambia, lolote mtakalolifunga duniani litakuwa limefungwa mbinguni, na lolote mtakalolifungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.
- Mathayo 18:19takriban 32 BK
“Tena nawaambia, ikiwa wawili wenu watakubaliana duniani kuhusu jambo lolote watakaloomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.
- Mathayo 18:20takriban 32 BK
Kwa kuwa wanapokusanyika pamoja watu wawili au watatu kwa Jina langu, mimi niko papo hapo pamoja nao.”
- Mathayo 18:21takriban 32 BK
Ndipo Petro akamjia Yesu na kumuuliza, “Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi nami nimsamehe? Je, hata mara saba?”
- Mathayo 18:22takriban 32 BK
Yesu akamjibu, “Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.
- Mathayo 18:23takriban 32 BK
“Kwa hiyo Ufalme wa Mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme aliyetaka kufanya hesabu zake za fedha na watumishi wake.
- Mathayo 18:24takriban 32 BK
Alipoanza kufanya hesabu zake, mtu mmoja aliyekuwa anadaiwa talanta10,000, aliletwa kwake.
- Mathayo 18:25takriban 32 BK
Kwa kuwa alikuwa hawezi kulipa deni hilo, bwana wake akaamuru kwamba auzwe, yeye, mkewe, watoto wake na vyote alivyokuwa navyo, ili lile deni lipate kulipwa.
- Mathayo 18:26takriban 32 BK
“Yule mtumishi akampigia magoti, akamsihi yule bwana akisema, ‘Naomba univumilie, nami nitakulipa deni lako lote.’
- Mathayo 18:27takriban 32 BK
Yule bwana wa huyo mtumishi akamwonea huruma, akafuta deni lake lote, akamwacha aende zake.
- Mathayo 18:28takriban 32 BK
“Lakini yule mtumishi alipokuwa anatoka nje, akakutana na mtumishi mwenzake aliyekuwa amemkopesha dinarimia moja. Akamkamata, akamkaba koo akimwambia, ‘Nilipe kile ninachokudai!’
- Mathayo 18:29takriban 32 BK
“Yule mtumishi mwenzake akapiga magoti akamsihi akisema, ‘Naomba univumilie, nami nitakulipa deni lako lote.’
- Mathayo 18:30takriban 32 BK
“Lakini akakataa. Badala yake, alienda akamtupa gerezani hata atakapolipa hilo deni.
- Mathayo 18:31takriban 32 BK
Watumishi wenzake walipoona haya yaliyotukia wakaudhika sana, nao wakaenda na kumwambia bwana wao kila kitu kilichokuwa kimetukia.
- Mathayo 18:32takriban 32 BK
“Yule bwana akamwita yule mtumishi akamwambia, ‘Wewe mtumishi mwovu! Mimi nilikusamehe deni lako lote uliponisihi.
- Mathayo 18:33takriban 32 BK
Je, haikukupasa kumhurumia mtumishi mwenzako kama mimi nilivyokuhurumia wewe?’
- Mathayo 18:34takriban 32 BK
Kwa hasira, yule bwana wake akamtia yule mtumishi mikononi mwa askari wa gereza ili ateswe mpaka atakapolipa yote aliyokuwa anadaiwa.
- Mathayo 18:35takriban 32 BK
“Hivi ndivyo Baba yangu wa mbinguni atakavyomfanyia kila mmoja wenu ikiwa hatamsamehe ndugu yake kutoka moyoni mwake.”
- Mathayo 19:1takriban 33 BK
Yesu alipomaliza kusema maneno haya, aliondoka Galilaya, akaenda sehemu za Uyahudi, ngʼambo ya Mto Yordani.
- Mathayo 19:2takriban 33 BK
Umati mkubwa wa watu ukamfuata, naye akawaponya huko.
- Mathayo 19:3takriban 33 BK
Baadhi ya Mafarisayo wakamjia ili kumjaribu, wakamuuliza, “Ni halali mtu kumwacha mke wake kwa sababu yoyote?”
- Mathayo 19:4takriban 33 BK
Akawajibu, “Je, hamkusoma kwamba hapo mwanzo Muumba aliwaumba mwanaume na mwanamke,
- Mathayo 19:5takriban 33 BK
naye akasema, ‘Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja’?
- Mathayo 19:6takriban 33 BK
Hivyo si wawili tena, bali mwili mmoja. Kwa hiyo alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.”
- Mathayo 19:7takriban 33 BK
Wakamuuliza, “Kwa nini basi Mose aliagiza mtu kumpa mkewe hati ya talaka na kumwacha?”