circa 6 BC – AD 30
The Life of Jesus
The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.
Mistari ya kipindi hiki
- Yohana 5:35takriban 31 BK
Yohana alikuwa taa iliyowaka na kutoa nuru, nanyi kwa muda mlichagua kuifurahia nuru yake.
- Yohana 5:36takriban 31 BK
“Lakini ninao ushuhuda mkuu zaidi kuliko wa Yohana. Kazi zile nizifanyazo, zinashuhudia juu yangu, zile ambazo Baba amenituma nizikamilishe, naam, ishara hizi ninazofanya, zinashuhudia kuwa Baba ndiye alinituma.
- Yohana 5:37takriban 31 BK
Naye Baba mwenyewe ameshuhudia juu yangu. Hamjapata kamwe kuisikia sauti yake wala kuona umbo lake,
- Yohana 5:38takriban 31 BK
wala hamna neno lake ndani yenu, kwa sababu hamkumwamini yeye aliyetumwa naye.
- Yohana 5:39takriban 31 BK
Ninyi mnachunguza Maandiko mkidhani ya kuwa ndani yake mna uzima wa milele, maandiko haya ndiyo yanayonishuhudia Mimi.
- Yohana 5:40takriban 31 BK
Lakini mnakataa kuja kwangu ili mpate uzima.
- Yohana 5:41takriban 31 BK
“Mimi sitafuti kutukuzwa na wanadamu.
- Yohana 5:42takriban 31 BK
Lakini ninajua kwamba hamna upendo wa Mungu mioyoni mwenu.
- Yohana 5:43takriban 31 BK
Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, nanyi hamnipokei, lakini mtu mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea.
- Yohana 5:44takriban 31 BK
Ninyi mwawezaje kuamini ikiwa mnapeana utukufu ninyi kwa ninyi, lakini hamna bidii kupata utukufu utokao kwa Mungu?
- Yohana 5:45takriban 31 BK
“Lakini msidhani kuwa mimi nitawashtaki mbele za Baba, mshtaki wenu ni Mose, ambaye mmemwekea tumaini lenu.
- Yohana 5:46takriban 31 BK
Kama mngelimwamini Mose, mngeliniamini na mimi kwa maana aliandika habari zangu.
- Yohana 5:47takriban 31 BK
Lakini ikiwa hamwamini aliyoandika Mose, mtaaminije ninayoyasema?”
- Yohana 6:1takriban 32 BK
Baada ya haya, Yesu alikwenda ngʼambo ya Bahari ya Galilaya, ambayo pia huitwa Bahari ya Tiberia.
- Yohana 6:2takriban 32 BK
Umati mkubwa wa watu uliendelea kumfuata, kwa sababu waliona ishara nyingi za miujiza alizofanya kwa wagonjwa.
- Yohana 6:3takriban 32 BK
Kisha Yesu akapanda mlimani akaketi huko pamoja na wanafunzi wake.
- Yohana 6:4takriban 32 BK
Pasaka ya Wayahudi ilikuwa imekaribia.
- Yohana 6:5takriban 32 BK
Yesu alipotazama na kuuona ule umati mkubwa wa watu ukimjia, akamwambia Filipo, “Tutanunua wapi mikate ili watu hawa wale?”
- Yohana 6:6takriban 32 BK
Aliuliza swali hili kumpima, kwa maana alishajua la kufanya.
- Yohana 6:7takriban 32 BK
Filipo akamjibu, “Hata fedha kiasi cha dinari mia mbili, hazitoshi kununua mikate ya kuwapa watu hawa ili kila mtu apate kidogo.”
- Yohana 6:8takriban 32 BK
Mmoja wa wanafunzi wake aitwaye Andrea, ndugu yake Simoni Petro, akamwambia,
- Yohana 6:9takriban 32 BK
“Hapa kuna mvulana mmoja mwenye mikate mitano ya shayiri na samaki wawili wadogo. Lakini hivi vitatosha nini kwa umati huu wote?”
- Yohana 6:10takriban 32 BK
Yesu akasema, “Waketisheni watu chini.” Palikuwa na majani mengi katika eneo lile, nao watu wakaketi. Palikuwa na wanaume wapatao 5,000.
- Yohana 6:11takriban 32 BK
Ndipo Yesu akachukua ile mikate, akamshukuru Mungu na kuwagawia wale watu waliokuwa wameketi. Akafanya vivyo hivyo na wale samaki. Kila mtu akapata kadiri alivyotaka.
- Yohana 6:12takriban 32 BK
Watu wote walipokwisha kula na kushiba, akawaambia wanafunzi wake, “Kusanyeni vipande vilivyobaki vya ile mikate, kisipotee chochote.”