circa 6 BC – AD 30
The Life of Jesus
The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.
Mistari ya kipindi hiki
- Luka 18:32takriban 33 BK
Kwa kuwa atatiwa mikononi mwa watu wasiomjua Mungu, nao watamdhihaki, watamtukana na kumtemea mate, watampiga mijeledi na kumuua.
- Luka 18:33takriban 33 BK
Naye siku ya tatu atafufuka.”
- Luka 18:34takriban 33 BK
Wanafunzi wake hawakuelewa mambo haya, kwa kuwa maana yake ilikuwa imefichika kwao, nao hawakujua Yesu alikuwa anazungumzia nini.
- Luka 18:35takriban 33 BK
Yesu alipokuwa anakaribia Yeriko, kipofu mmoja alikuwa ameketi kando ya njia akiomba msaada.
- Luka 18:36takriban 33 BK
Kipofu huyo aliposikia umati wa watu ukipita, akauliza, “Kuna nini?”
- Luka 18:37takriban 33 BK
Wakamwambia, “Yesu wa Nazareti anapita.”
- Luka 18:38takriban 33 BK
Akapaza sauti, akasema, “Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!”
- Luka 18:39takriban 33 BK
Wale waliokuwa wametangulia mbele wakamkemea, wakamwambia akae kimya. Lakini yeye akapaza sauti zaidi, “Mwana wa Daudi, nihurumie!”
- Luka 18:40takriban 33 BK
Yesu akasimama, akawaamuru wamlete huyo mtu kwake. Alipokaribia, Yesu akamuuliza,
- Luka 18:41takriban 33 BK
“Unataka nikufanyie nini?” Akajibu, “Bwana, nataka kuona.”
- Luka 18:42takriban 33 BK
Yesu akamwambia, “Basi upate kuona. Imani yako imekuponya.”
- Luka 18:43takriban 33 BK
Akapata kuona saa ile ile, akamfuata Yesu, huku akimsifu Mungu. Watu wote walipoona mambo hayo, nao wakamsifu Mungu.
- Luka 19:1takriban 33 BK
Yesu akaingia Yeriko, naye alikuwa anapita katikati ya huo mji.
- Luka 19:2takriban 33 BK
Tazama, palikuwa na mtu mmoja mkuu wa watoza ushuru naye alikuwa tajiri, jina lake Zakayo.
- Luka 19:3takriban 33 BK
Yeye alikuwa akijitahidi kumwona Yesu ni mtu wa namna gani. Lakini kutokana na umati mkubwa wa watu hakuweza kwa sababu alikuwa mfupi wa kimo.
- Luka 19:4takriban 33 BK
Kwa hiyo akatangulia mbio mbele ya umati wa watu akapanda juu ya mkuyu ili amwone Yesu, kwa sababu angeipitia njia ile.
- Luka 19:5takriban 33 BK
Yesu alipofika pale chini ya huo mkuyu, akatazama juu, akamwambia, “Zakayo, shuka upesi, kwa maana leo nitakuwa mgeni nyumbani kwako!”
- Luka 19:6takriban 33 BK
Hivyo Zakayo akashuka upesi, akamkaribisha Yesu nyumbani kwake kwa furaha kubwa.
- Luka 19:7takriban 33 BK
Watu wote walipoona hivyo, wakaanza kunungʼunika wakisema, “Amekwenda kuwa mgeni wa ‘mtu mwenye dhambi.’ ”
- Luka 19:8takriban 33 BK
Lakini Zakayo akasimama na kumwambia Bwana, “Tazama, Bwana! Sasa hivi nusu ya mali yangu ninawapa maskini, nami kama nimemdhulumu mtu yeyote kitu chochote, nitamrudishia mara nne ya hicho kiwango.”
- Luka 19:9takriban 33 BK
Ndipo Yesu akamwambia, “Leo, wokovu umeingia nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Abrahamu.
- Luka 19:10takriban 33 BK
Kwa maana Mwana wa Adamu amekuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.”
- Luka 19:11takriban 33 BK
Walipokuwa wanasikiliza haya, Yesu akaendelea kuwaambia mfano, kwa sababu alikuwa anakaribia Yerusalemu na watu walikuwa wakidhani ya kuwa Ufalme wa Mungu ulikuwa unakuja saa iyo hiyo.
- Luka 19:12takriban 33 BK
Hivyo akawaambia: “Mtu mmoja mwenye cheo kikubwa alisafiri kwenda nchi ya mbali ili akapokee madaraka ya kuwa mfalme, kisha arudi.
- Luka 19:13takriban 33 BK
Hivyo akawaita kumi miongoni mwa watumishi wake, na akawapa kila mmoja fungu la fedha. Akawaambia, ‘Fanyeni biashara na fedha hizi mpaka nitakaporudi.’