Rukia maudhui

circa 605–538 BC

The Babylonian Exile

Jerusalem falls and the temple burns; Ezekiel and Daniel minister among the exiles as Lamentations mourns the city's ruin.

1,784 mistari · 3 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Ezekieli 37:14takriban 587 KK

    Nitatia Roho yangu ndani yenu nanyi mtaishi, nami nitawakalisha katika nchi yenu wenyewe. Ndipo mtakapojua kwamba Mimi Bwana nimenena, nami nitalitenda, asema Bwana!’ ”

  2. Ezekieli 37:15takriban 587 KK

    Neno la Bwana likanijia kusema:

  3. Ezekieli 37:16takriban 587 KK

    “Mwanadamu, chukua fimbo na uandike juu yake, ‘Hii ni kwa ajili ya Yuda na Waisraeli waliofungamana naye.’ Kisha chukua fimbo nyingine, uandike juu yake, ‘Fimbo ya Efraimu, ni kwa ajili ya Yosefu na nyumba yote ya Israeli wanaofungamana naye.’

  4. Ezekieli 37:17takriban 587 KK

    Ziunganishe pamoja kuwa fimbo moja ili kwamba ziwe fimbo moja katika mkono wako.

  5. Ezekieli 37:18takriban 587 KK

    “Watu wako watakapokuuliza, ‘Je, hutatuambia ni nini maana ya jambo hili?’

  6. Ezekieli 37:19takriban 587 KK

    Waambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitaichukua fimbo ya Yosefu, iliyoko mikononi mwa Efraimu na ya makabila ya Israeli yanayofungamana naye na kuiunganisha na fimbo ya Yuda, nikizifanya kuwa fimbo moja, nao watakuwa wamoja katika mkono wangu.’

  7. Ezekieli 37:20takriban 587 KK

    Inua mbele ya macho yao zile fimbo ulizoziandika

  8. Ezekieli 37:21takriban 587 KK

    kisha waambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitawatoa Waisraeli katika mataifa walikokuwa wamekwenda. Nitawakusanya popote walipo na kuwarudisha katika nchi yao wenyewe.

  9. Ezekieli 37:22takriban 587 KK

    Nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi, katika milima ya Israeli. Patakuwa na mfalme mmoja juu yao wote na kamwe hawatagawanyika tena kuwa mataifa mawili au kugawanyika katika falme mbili.

  10. Ezekieli 37:23takriban 587 KK

    Hawatajitia tena unajisi kwa sanamu zao na vinyago vyao visivyo na maana wala kwa makosa yao yoyote, kwa maana nitawaokoa kutoka dhambi zao zote zilizowarudisha nyuma, nami nitawatakasa. Wao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.

  11. Ezekieli 37:24takriban 587 KK

    “ ‘Mtumishi wangu Daudi atakuwa mfalme juu yao, nao wote watakuwa na mchungaji mmoja. Watafuata sheria zangu na kuzishika amri zangu kwa uangalifu.

  12. Ezekieli 37:25takriban 587 KK

    Wataishi katika nchi niliyompa mtumishi wangu Yakobo, nchi ambamo baba zenu waliishi. Wao na watoto wao na watoto wa watoto wao wataishi humo milele, naye Daudi mtumishi wangu atakuwa mkuu wao milele.

  13. Ezekieli 37:26takriban 587 KK

    Nitafanya nao Agano la amani, litakuwa Agano la milele. Nitawafanya imara na kuongeza idadi yao, nami nitaweka mahali patakatifu pangu miongoni mwao milele.

  14. Ezekieli 37:27takriban 587 KK

    Maskani yangu yatakuwa pamoja nao, nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

  15. Ezekieli 37:28takriban 587 KK

    Ndipo mataifa watakapojua kwamba Mimi Bwana ndiye ninayeifanya Israeli kuwa takatifu, wakati mahali patakatifu pangu patakapokuwa miongoni mwao milele.’ ”

  16. Ezekieli 38:1takriban 587 KK

    Neno la Bwana likanijia kusema:

  17. Ezekieli 38:2takriban 587 KK

    “Mwanadamu, kaza uso wako dhidi ya Gogu, katika nchi ya Magogu, mkuu wa Roshi, Mesheki na Tubali, tabiri dhidi yake

  18. Ezekieli 38:3takriban 587 KK

    na useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ee Gogu, mimi ni kinyume nawe, mtawala mkuu wa Roshi, Mesheki na Tubali.

  19. Ezekieli 38:4takriban 587 KK

    Nitakugeuza kuelekea ulikotoka na kukutia ndoana kwenye mataya yako na kukutoa nje wewe pamoja na jeshi lako lote, yaani, farasi wako, wapanda farasi wako waliojiandaa tayari kwa vita, pamoja na kundi kubwa la wajeuri wakiwa na ngao na vigao, wote wakipunga panga zao.

  20. Ezekieli 38:5takriban 587 KK

    Uajemi, Kushi na Putu watakuwa pamoja nao, wote wakiwa na ngao na kofia za chuma,

  21. Ezekieli 38:6takriban 587 KK

    pia Gomeri pamoja na vikosi vyake vyote, na Beth-Togarma kutoka kaskazini ya mbali pamoja na vikosi vyake vyote, mataifa mengi wakiwa pamoja nawe.

  22. Ezekieli 38:7takriban 587 KK

    “ ‘Jiandae, uwe tayari, wewe na makundi yako yote ya wajeuri yaliyokusanyika pamoja nawe, nawe waamrishe.

  23. Ezekieli 38:8takriban 587 KK

    Baada ya siku nyingi utaitwa vitani. Katika miaka ijayo, utaivamia nchi ile ambayo imepona kutoka vita, ambayo watu wake walikusanywa kutoka mataifa mengi kuja katika milima ya Israeli, ambayo kwa muda mrefu ilikuwa imeachwa ukiwa. Wameletwa kutoka mataifa na sasa wote wanaishi katika hali ya salama.

  24. Ezekieli 38:9takriban 587 KK

    Wewe na vikosi vyako vyote na mataifa mengi yaliyo pamoja nawe mtapanda juu, mtawazoa kama tufani na kuifunika nchi kama wingu.

  25. Ezekieli 38:10takriban 587 KK

    “ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Katika siku ile mawazo yataingia moyoni mwako nawe utapanga mipango mibaya.