Rukia maudhui

circa 1446 BC

Sinai & The Law

God meets Israel at Mount Sinai, reveals the Ten Commandments, and establishes the Tabernacle and the priestly covenant.

1,657 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Walawi 25:54takriban 1491 KK

    “ ‘Hata ikiwa hakukombolewa kwa njia mojawapo ya hizi, yeye na watoto wake wataachiwa katika Mwaka wa Yubile,

  2. Walawi 25:55takriban 1491 KK

    kwa maana Waisraeli ni mali yangu kama watumishi. Wao ni watumishi wangu, niliowatoa kutoka nchi ya Misri. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.

  3. Walawi 26:1takriban 1491 KK

    “ ‘Msijitengenezee sanamu au kusimamisha kinyago cha kuchonga, au mnara, wala jiwe la kuabudia, na pia msijiwekee jiwe lililochongwa katika nchi yenu na kusujudu mbele yake. Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.

  4. Walawi 26:2takriban 1491 KK

    “ ‘Zishikeni Sabato zangu na kuheshimu mahali patakatifu pangu. Mimi ndimi Bwana.

  5. Walawi 26:3takriban 1491 KK

    “ ‘Ikiwa mtafuata amri zangu na kuwa waangalifu kutii maagizo yangu,

  6. Walawi 26:4takriban 1491 KK

    nitawanyeshea mvua katika majira yake, nayo ardhi itatoa mazao yake, na miti ya mashambani itazaa matunda yake.

  7. Walawi 26:5takriban 1491 KK

    Kupura nafaka kwenu kutaendelea mpaka wakati wa kuvuna zabibu. Pia kuvuna zabibu kutaendelea mpaka wakati wa kupanda mbegu, nanyi mtakula na kushiba, na mtaishi salama katika nchi yenu.

  8. Walawi 26:6takriban 1491 KK

    “ ‘Nitawapa amani katika nchi, mpate kulala pasipo kutiwa hofu na yeyote. Nitawaondoa wanyama wakali watoke kwenye nchi, nao upanga hautapita katika nchi yenu.

  9. Walawi 26:7takriban 1491 KK

    Mtawafukuza adui zenu, nanyi mtawaua kwa upanga mbele yenu.

  10. Walawi 26:8takriban 1491 KK

    Watu wenu watano watafukuza adui mia, watu wenu mia watafukuza adui elfu kumi, nao adui zenu wataanguka kwa upanga mbele yenu.

  11. Walawi 26:9takriban 1491 KK

    “ ‘Nitawaangalia kwa upendeleo na kuwafanya mzae na kuzidisha idadi yenu, nami nitalishika Agano langu na ninyi.

  12. Walawi 26:10takriban 1491 KK

    Wakati wa kuvuna mtakuwa bado mnakula mavuno ya mwaka uliopita, na itawalazimu kuyaondoa ghalani ili mpate nafasi ya mavuno mapya.

  13. Walawi 26:11takriban 1491 KK

    Nitafanya makao yangu miongoni mwenu, nami sitawachukia.

  14. Walawi 26:12takriban 1491 KK

    Nitatembea katikati yenu niwe Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu.

  15. Walawi 26:13takriban 1491 KK

    Mimi ndimi Bwana Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri ili msiendelee kuwa watumwa wa Wamisri, nikavunja kongwa lenu, na kuwawezesha kutembea mkiwa mmeinua vichwa vyenu juu.

  16. Walawi 26:14takriban 1491 KK

    “ ‘Lakini kama hamtanisikiliza na kutimiza maagizo haya yote,

  17. Walawi 26:15takriban 1491 KK

    nanyi kama mtazikataa amri zangu na kuzichukia sheria zangu, tena mkishindwa kutimiza amri zangu na hivyo mkavunja agano langu,

  18. Walawi 26:16takriban 1491 KK

    ndipo nitakapowafanyia hili: Nitawaletea juu yenu hofu ya ghafula, magonjwa ya kufisha, na homa itakayopofusha macho yenu na kuwaondolea uhai wenu. Mtapanda mbegu bila mafanikio, kwa sababu adui zenu wataila.

  19. Walawi 26:17takriban 1491 KK

    Nitauelekeza uso wangu dhidi yenu ili mshindwe na adui zenu; wale wanaowachukia watawatawala, nanyi mtakimbia ingawa hakuna mtu anayewafukuza.

  20. Walawi 26:18takriban 1491 KK

    “ ‘Kama baada ya haya yote hamtanisikiliza, nitawaadhibu mara saba zaidi kwa ajili ya dhambi zenu.

  21. Walawi 26:19takriban 1491 KK

    Nitakivunja kiburi chenu cha ukaidi na kuifanya anga iliyo juu yenu iwe kama chuma, na ardhi yenu kama shaba.

  22. Walawi 26:20takriban 1491 KK

    Nguvu zenu zitatumika bila ya mafanikio, kwa sababu ardhi yenu haitawazalia mazao yake, wala miti ya nchi yenu haitazaa matunda yake.

  23. Walawi 26:21takriban 1491 KK

    “ ‘Kama mtaendelea kuwa na uadui nami, na kukataa kunisikiliza, nitawazidishia mateso yenu mara saba zaidi, kama dhambi zenu zinavyostahili.

  24. Walawi 26:22takriban 1491 KK

    Nitawatuma wanyama mwitu dhidi yenu, nao watawaibieni watoto wenu, watawaangamiza ngʼombe wenu, na kuifanya idadi yenu kuwa ndogo, hivi kwamba barabara zenu zitakuwa hazina watu.

  25. Walawi 26:23takriban 1491 KK

    “ ‘Ikiwa pamoja na mambo haya hamtakubali maonyo yangu lakini mkaendelea kuweka uadui nami,